HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, September 27, 2023

ATARE yaweka mikakati kwa watafiti nchini

*Yabainisha moja ya mikakati kutafuta rasilimali fedha ya utafiti

Na Chalila Kibuda, Michuzi TV

CHAMA Cha Watafiti Tanzania (ATARE),kimesema kuwa maendeleo ya nchi yeyote yalipatikana kwa ajili ya kuweka mbele masuala mbalimbali kwa kufanya utafiti

"Hakuna nchi yoyote duniani iliyopata maendeleo bila ya kufanya tafiti  hivyo ni muhimu kuwekeza katika eneo hilo kwa serikali yetu kuweka suala la utafiti kupewa kipaumbele" amesema Rais wa ATARE Prof.Ndunguru.

Hayo yamebainishwa jijini Dar es salaam na Raiswa ATARE ambaye pia ni Mwanzilishi wa Chama hicho ,Profesa Joseph Ndunguru wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu kuanzishwa kwa Chama hicho kwa watafiti kujunga na  Chama hicho Jijini Dar es Salaam.


"Tunapoongelea uchumi wa viwanda lazima kuwe na utafiti ambao unalenga kuboresha bidhaa zinazozalishwa viwanda kwa kuangalia mahitaji ya ndani na nje ya nchi kwa kutumia utafiti"amesema Profesa Ndunguru.

Amesema utafiti ni kitu muhimu katika maendeleo ya nchi kwasababu kupitia tafiti kunaweza kuleta suluhu ya mambo mbalimbali ikiwemo kutibu magonjwa mbalimbali.

Aliongeza kuwa malengo mahususi ya chama hicho ni kuanzisha ushirikiano ambao itaisaidia wanachama wake katika kuanzisha na kuendeleza mipango mbalimbali ya utafiti na kuweka kumbukumbu za tafiti zilizofanywa.

"Ili uweze kuwa mtafiti mzuri ni lazima ushirikiano na Watafiti wengine nje na ndani ya nchi hivyo Chama hiki kitakuwa kinasaidia kuratibu hayo cha msingi ni warafiti wajiunge"alisisitiza Profesa Ndunguru.

Prifesa Ndunguru amesema  Chama hicho kitaamasisha ufanyanyaji wa tafiti za kisayansi na kuongeza usambazaji taarifa na maarifa kwa maendeleo endelevu.

Amesema kupitia Chama hicho kutaanzishwa  mfuko wa rasilimali fedha zitakazotoka katika vyanzo mbalimbali kwa ajili ya kusaidia miradi ya tafiti kwa wanachama wake.

"Utafiti unahitaji fedha nyingi na mara nyingi Serikali pekee yake haiwezi kutafutia fedha za kutosheleza utafiti hivyo kupitia Chama hiki tutakitumia kutafuta vyanzo vya fedha kwa ajili ya wanachama wake ili waweze kuendeleza tafiti zao,"amesema Profesa Nduguru.

Hata hivyo amesema ATARE itakuwa na utaratibu wa  kuwajengea uwezo watafiti vijana na wanawake na wanaoibukia katika fani hiyo ili kukabiliana na changamoto mbalimbali.

Aidha  alitoa wito kwa watafiti kujiunga na Chama hicho ili waweze kukuza uchumi wa nchi kupitia tafiti.


"Hiki ni Chama cha kwanza cha Watafiti na  wazo hili limetokana na watanzania wenyewe kwa ajili ya kutatua chagamoto za watafiti hivyo hii ndio fursa ya watafiti kujiunga na ATARE,"amesema Profesa Ndunguru.

Aliongeza kuwa "kupitia Chama hiki tutaweza kuibua fursa ikiwa ni pamoja kuishauri serikali,"aliongeza. Rais wa Chama cha Watafiti Tanzania(ATARE)Profesa Joseph Ndunguru akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na kuanzishwa kwa chama hicho jijini Dar es Salaam.

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa ATARE  Geoffrey Kirenga  akizungumza kuhusiana na mipango iliyowekwa katika bodi ya ATARE , Jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad