TCD WAKAA NA VIONGOZI WA JUMUIYA YA WANAWAKE KUJADILI NAMNA YA KUANZISHA JUKWAA LAO - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, August 9, 2023

TCD WAKAA NA VIONGOZI WA JUMUIYA YA WANAWAKE KUJADILI NAMNA YA KUANZISHA JUKWAA LAO

 KITUO cha Demokrasia Tanzania (TCD) kimefanya kikao na viongozi wa Jumuiya za wanawake wa vyama wanachama wa TCD kujadili namna ya kuanzisha jukwaa la wanawake chini ya Kituo hicho.


Kikao hicho kimefanyika katika ofisi za Kituo cha Demokrasia Tanzania zilizopo Mikocheni jijini Dar es Salaam leo Agosti 09, 2023 huku vyama; CHADEMA, CCM, CUF, ACT-WAZALENDO pamoja na NCCR - Mageuzi wakishiriki.

CHAUMMA wameshiriki kuwakilisha vyama visivyo na wabunge/madiwani.

Jukwaa hilo linaundwa ili kuwakutanisha pamoja viongozi wa Jumuiya za wanawake za vyama wanachama wa TCD kujadili masuala mbalimbali yanayolenga kutatua changamoto za wanawake katika siasa na uongozi.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad