NA EMMANUEL MBATILO, MICHUZI TV
CHAMA cha Waajiri Tanzania 
(ATE) kwa kushirikiana na Shirika la Kazi Duniani (ILO) wameandaa 
mkutano wa majadiliano wa sekta binafsi na wadau kujadili mchango wa 
sekta binafsi katika kuzuia maambukizi ya UKIMWI katika Maeneo ya Kazi.
Akizungumza
 katika Mkutano huo leo Augosti 9,2023 Jijini Dar es Salaam, Mtendaji 
Mkuu wa ATE, Bi. Suzanne Ndomba amesema uwepo wa mkutano huo ni katika 
kutekeleza mpango mkakati wa Dunia wa kumaliza janga la UKIMWI ifikapo 
mwaka 2030.
Amesema mchango mkubwa unaotolewa na ATE katika 
kuzikutanisha Sekta Binafsi na Wadau kupitia Programu mbalimbali za afya
 na masuala ya UKIMWI katika maeneo ya Kazi kwa kuzingatia Dunia iko 
katika mpango mkakati wa kumaliza janga la UKIMWI ifikapo mwaka  2030. 
"Pamoja
 na hatua kubwa ambazo Tanzania imepiga katika kutokomeza  UKIMWI,  bado
 kuna kazi kubwa ya kufanya na wadau wote ili kupata Tanzania isiyo na 
VVU/UKIMWI na kuwa  ATE kwa kushirikiana na Serikali na Wadau wengine 
wataendelea kuunga mkono juhudi zote za kufikia lengo ifikapo mwaka 
2030". Amesema Bi.Suzanne
Naye Katibu Mkuu wa Shirikisho la Vyama
 vya Wafanyakazi Nchini ( TUCTA), Bw. Herry Mkunda ambaye pamoja na 
mambo mengine amewaomba wadau wote kuendeleza ushirikiano katika 
kuhamasisha  masuala ya UKIMWI na Afya na Usalama mahala pa Kazi ili 
kufikia malengo ya mkakati wa 95% hadi kufikia mwaka 2030. 
"Katika
 sehemu ya kazi tunatakiwa tulinde  wafanyakazi kwasababu muajiri hawezi
 kupata faida kama wafanyakazi hawana afya nzuri kwahiyo pamoja na mambo
 mengine isiwe UKIMWI pekee bali hata magonjwa mengine yasiyoambukiza, 
hii itaweza kuondoa changamoto ya Afya sehemu ya kazi" Amesema 
Pamoja
 na hayo amewaomba waajiri kuhakikisha wanaweka mipango ya kupambana na 
UKIMWI sehemu za kazi kama sehemu za bajeti zao lakini pia kuwe na 
utaratibu maalumu wa kupambana na magonjwa yasiyo ya kuambukiza"
Kwa
 upande wake Afisa Program Mwandamizi kutoka Shirika la Kazi Duniani 
Kanda ya Afrika Mashariki (ILO),Edmund Moshi alisema katika utekelezaji 
wa afya mbalimbali za eneo la afya bado kuna mambo mengi ya kufanya 
ikiwemo kuendeleza juhudi za kuhakikisha kwamba UKIMWI unaisha lakini 
pia pale ambapo upo watu wanaendelea kupewa msaada wanaohitaji ili 
kuendelea kuwa na Tija mahali pa kazi.
Mkutano huo umebeba kauli 
mbiu inayosema *“UKIMWI bado ni Ajenda Endelevu” yaani “AIDS is an 
unfinished Business.” Mkutano huu, Utatafuatiwa na mafunzo ya siku tatu 
wa Wakufunzi wa Rika “Peer Educators Training” yenye lengo la kuwajengea
 uwezo kuhusiana na masala ya UKIMWI na Afya katika maeneo ya kazi. 
Hata
 hivyo Mafunzo hayo yamebeba kaulimbiu inayosema “Mafunzo kwa 
Waelimishaji Rika katika Maeneo ya Kazi ni Msingi Endelevu katika 
mapambano dhidi ya UKIMWI: Wakati ni sasa” yaani Workplace Peer 
Education is Key for Sustainability of HIV/Wellness Programs: Time to 
Act!”
Na vilevile Mkutano huo umehudhuriwa pia na Mkurugenzi 
Mkaazi wa UNAIDs, Dkt. Martin. Ordiit, Mwakilishi kutoka Tume ya Taifa 
ya Kudhibiti UKIMWI ( TACAIDs), Mwakilishi kutoka  Ofisi ya Kamishna  wa
 Kazi pamoja na wadau mbalimbali wa Masuala ya UKIMWI kutoka ndani na 
nje ya Nchi.
Mkutano wa majadiliano wa sekta binafsi na wadau kujadili mchango wa sekta binafsi katika kuzuia maambukizi ya UKIMWI katika Maeneo ya Kazi. Mkutano huo umefanyika leo Augosti 9,2023 Jijini Dar es Salaam
Mtendaji Mkuu wa ATE, Bi. Suzanne Ndomba akizungumza katika mkutano wa majadiliano wa sekta binafsi na wadau kujadili mchango wa sekta binafsi katika kuzuia maambukizi ya UKIMWI katika Maeneo ya Kazi. Mkutano huo umefanyika leo Augosti 9,2023 Jijini Dar es Salaam
Katibu Mkuu wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Nchini ( TUCTA), Bw. Herry Mkunda akizungumza katika mkutano wa majadiliano wa sekta binafsi na wadau kujadili mchango wa sekta binafsi katika kuzuia maambukizi ya UKIMWI katika Maeneo ya Kazi. Mkutano huo umefanyika leo Augosti 9,2023 Jijini Dar es SalaamAfisa Program Mwandamizi kutoka Shirika la Kazi Duniani Kanda ya Afrika Mashariki (ILO), Bw. Edmond Moshi akizungumza katika mkutano wa majadiliano wa sekta binafsi na wadau kujadili mchango wa sekta binafsi katika kuzuia maambukizi ya UKIMWI katika Maeneo ya Kazi. Mkutano huo umefanyika leo Augosti 9,2023 Jijini Dar es Salaam
Wadau mbalimbali kutoka sekta binafsi wakiwa kwenye mkutano wa majadiliano wa sekta binafsi na wadau kujadili mchango wa sekta binafsi katika kuzuia maambukizi ya UKIMWI katika Maeneo ya Kazi. Mkutano huo umefanyika leo Augosti 9,2023 Jijini Dar es Salaam
(PICHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO)

No comments:
Post a Comment