IAA kutoa udhamini kwa shahada ya kwanza - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, August 24, 2023

IAA kutoa udhamini kwa shahada ya kwanza

*Kimejipanga katika kufikia ndoto ya Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan

Chuo cha Uhasibu Arusha (IAA) umepanga kuanza kutoa  kutoa udhamini wanafunzi 40 wa masomo ngazi ya shahada  ya kwanza katika mwaka wa masomo 2023/24 kwa wale wenye sifa  za kupata udhamini huo.

Chuo hicho kimesema kutokana na uwepo wa wimbi la watu wenye ndoto za kusoma lakini wanakabiliwa na ukosefu wa fedha wameamua kutumia fursa hiyo ambayo itawanufaisha watanzania.

Akizungumza na waandishi wa habari katika Tawi la IAA lililopo jijini Dar es Salaam Mkuu wa Chuo hicho, Profesa Eliamani Sedoyeka amesema kifanya hivyo ni kuunga mkono juhudi za serikali ya awamu ya sita ya Rais Dkt.Samiia Suluhu Hassan  kutoa udhamini wa elimu.

"Rais Dkt.  Samia Suluhu Hassan  ametoa udhamini wa masomo kwa wanafunzi wa masomo ya sayansi (Samia Scholarship), Sisi kama Taasisi ya elimu ya juu tumeamua kuunga mkono katika kutoa udhamini wa masomo katika fani zetu mpya," amesema Sedoyeka.

Amesema fani watazotoa udhamini ni  Shahada ya Ukaguzi wa Hesabu na Uhakikisho, Shahada ha Media Unuwai na Mawasiliano kwa umma, Shahada ya Usimamizi wa Nyaraka na Taarifa, Shahada ya Usimamizi wa Mkopo, pamoja na Shahada ya Ukutubi na Sayansi ya Taarifa.

Profesa Sedoyeka amesema  katika  kuhakikishaa hilo wahitimu wa kidato cha sita wa mwaka 2022/23 wenye ndoto na malengo ya kusomea kozi tajwa na wale wanaokabiriwa na changamoto ya kifedha lakini  hiyo hatoshi kuna sifa ziada kwenye maombi ya udhamini huo.

Amesema wanahitajika wawe na ufaulu mzuri wa kidato cha nne na kidato cha sita pamoja na nia ya dhati ya kusoma kozi hizo.

Amesema Chuo hicho kina kozi 70 ambapo watanzania wanaendelea kunufaika na kuleta tija katika Taifa.

Profesa amesema kuwa katika kupanua utoaji wa elimu wanakwenda kufugua tawi Mkoa Ruvuma ili kuwafikia watanzania kila kona ya nchi.

Mkuu wa Chuo cha Uhasibu Arusha (IAA) Profesa Eliamani Sedoyeka akizungumza na waandishi habari kuhusiana na chuo hicho kutoa udhamini wa masomo kwa mwaka wa masomo 2023/2024 jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad