GF Vehicle Assemblers(GFA) yang’ara tuzo za Africa Company of the year 2023, - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Saturday, August 5, 2023

GF Vehicle Assemblers(GFA) yang’ara tuzo za Africa Company of the year 2023,

 
Kampuni ya Gf Trucks & Equipment’s Ltd imeibuka mshindi wa Tuzo za ACOYA 2023 kwa Uzaaji wa Magari nchini Tanzania na Unganishaji kupitia Kiwanda cha GF Vehicle Assemblers(GFA) kilichopo Kibaha mkoani Pwani

Tuzo za Kampuni Bora ya Afrika (ACOYA) zilizoandaliwa na Estern Star Consulting Group zilishirikisa makampuni mbalimbali nchini zimefanyika jijini Dar es salaam .

Akizungumza wakati wa utoaji wa tuzo hizo Mkurugenzi wa Masoko na Mawasiliano wa kampuni ya GF ,Salman Karmal alisema wao wanajivunia kuchukua tuzo hizo mbili kwa kupitia Kiwanda chao cha uunganishaji wa Magari kilichopo Kibaha na uuzaji wa magari makubwa (trucks)

Kutokana na mazingira mazuri ya serikali kwa wawekezaji tumekuwa tukifanya vizuri siku hadi siku na kwa sasa Kiwanda chetu cha GFA kilichopo Kibaha mkoani Pwani kipo katika awamu ya pili ya upanuzi na tunategemea kuongeza uzalishaji kutoka Magari 1800 mpaka 2500 wa mwaka huu

Hii inatokana na malengo yetu tuliojiwekea kulifikia soko la Afrika mashariki na kati kwani nchi kama Kongo,Zambia Randa na Burundi ni miongoni mwa wateja wetu wakuu kwa upande wa magari makubwa katika sekta ya usafirishaji

Kiwanda chetu cha GFA kinaunganisha magari aina ya FAW, HONG YANG na FORAND hali inayosababisha magari hayo kwa sasa kupatikana kwa bei nafuu ukilinganisha na hapo zamani

Pia kwa GF tuzo hizi tunazipeleka kwa wakazi wa maeneo ya Kibaha sehemu ambayo kiwanda kipo kwa kuwaandalia mzuri ya kusherehekea pamoja unajua ukiwa na furaha basi ili furaha ikamilike unatakiwa kuwa pamoja na marafiki zako kwetu marafiki wa tuzo hii ni Wadau,wateja wakazi wa mkoa wa Kibaha na awafanyakazi kunajambo kubwa la kijamii linakuja alimaliza Karmal.

Nae mkurugenzi wa Africa Company of The Year Awards (ACOYA), Deogratius Kilawe ambao ni waandaji wa tuzo hizo alizipongeza na kuzishukuru kampuni zote zilizoshiriki na kushida na kusema kuwa lengo la tuzo hizo ni makampuni ni kuweza kuongeza ufanisi katika kutoa huduma kwa wateja wao na wafanyakazi ili kuongeza uwajibikaji kazini mwisho wa tuzo hizi ni mwanzo wa maandalizi wa tuzo zijazo tunachukua chamgamoto zilizojitokeza mwaka huu kuboresha Tuzo zijazo.
Mkurugenzi Mtendaji Kiwanda ya GF Vehicle Assemblers Limited, Imran Karmali , Meneja Mkuu wa kiwanda hicho , Ezra Mereng (kushoto)Meneja Uzalishaji , Laban Dundo(wa pili kulia) na Kulia ni mkaguzi wa mahesabu wa ndani Akberali Khakoo kwa pamoja wakiwa wameshika tuzo za Kampuni Bora ya Afrika (ACOYA) kwa uunganishaji(Assemblers) na uuzaji wa magari iliyofanyika jijini Dar es salaam.

tuzo
Mkurugenzi Mtendaji Kiwanda ya GF Vehicle Assemblers Limited, Imran Karmali(kulia) na Meneja Mkuu wa kiwanda hicho , Ezra Mereng wakifrahi pamoja baada ya kuibuka na tuzo mbili
Wafanyakazi wa kampuni ya GF Trucks wakifurahia pamoja baada ya kupokea  Tuzo

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad