RC CHALAMILA AMUAPISHA DC MPYA TEMEKE - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, July 4, 2023

RC CHALAMILA AMUAPISHA DC MPYA TEMEKE

Mkuu wa Wilaya ya Temeke Mobhare Holmes Matinyi akila kiapo mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Albert Chalamila leo asubuhi Julai 4 2023 katika hafla ya uapisho iliyofanyika kwenye Ukumbini wa Mikutano ofisini kwa RC. RC Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Albert Chalamila akimkabidhi Mkuu wa Wilaya ya Temeke Mobhare Holmes Matinyi ilani ya CCM na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mara baada ya kuapishwa.

Mkuu wa Wilaya ya Temeke Mobhare Holmes Matinyi akisaini hati ya kiapo baada ya kuapishwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Albert Chalamila.

Na Khadija Kalili Michuzi TV
MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam Mheshimiwa Albert Chalamila leo Julai 4 2023 asubuhi amemuapisha Mkuu wa Wilaya ya Temek Mheshimiwa Mobhare Holmes Matinyi .

Uapisho huo ni kufuatia uteuzi uliofanywa hivi karibuni na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Mheshimiwa Dkt Samia Suluhu Hassan.

Hafla ya Uapisho huo imefanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Ofisi ya Mkoa huo Ilala Jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na Viongozi mbalimbali wa Sekretarieti na Wilaya za Mkoa huo wakiongozwa na

Katibu Tawala wa Mkoa Bi Rehema Madenge ikiwemo Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa.

RC Chalamila memtakia majukumu mema DC Matinyi katika kuwahudumia wananchi wa Wilaya ya Temeke huku akitoa rai kwa Viongozi wa Manispaa na Wilaya kumpa ushirikiano kiongozi huyo.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad