KATIBU MKUU NISHATI ATEMBELEA BANDA LA EWURA SABASABA - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, July 4, 2023

KATIBU MKUU NISHATI ATEMBELEA BANDA LA EWURA SABASABA

Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Mhandisi Felchesmi Mramba, akisikiliza maelezo kutoka kwa Meneja wa Mawasiliano na Uhusiano wa EWURA, Bw. Titus Kaguo (wapili kulia), alipotembelea banda la EWURA katika maonesho ya 47 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba), leo Tar. 3.07.2023. Kulia ni Ofisa Uhusiano Mwandamizi wa EWURA, Bi. Asiatu Msuya na kushoto ni Ofisa Uhusiano wa EWURA Bi. Tobietha Makafu.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Mhandisi Felchesmi Mramba akisaini kitabu banda la EWURA, alipotembelea banda la katika maonesho ya 47 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea katika viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere Sabasaba jijini Dar es Salaam.

KATIBU wa Wizara ya Nishati Mhandisi Felschimi Mramba ametembelea Banda la Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) katika Maonesho ya 47 ya Biashara ya Kimataifa Dar es Salaam( DITF) yanayoendelea Viwanja Vya Mwalimu Julius Nyerere, maarufu Sabasaba, Jijini Dar es Salaam.

Meneja Uhusiano na Mawasiliano EWURA, Titus Kaguo, amemweleza Kiongozi huyo kuwa, EWURA imejipanga kuelimisha wananchi kuhusu namna ya kufanya maombi ya leseni kidijiti na namna EWURA inavyotekeleza majukumu yake ya udhibiti wa huduma za nishati na maji.

Aidha Bw.Kaguo ameeleza kuwa, ushiriki wa EWURA katika maonesho hayo utatoa fursa kwa Mamlaka kusikiliza, kutoa mwongozo na kutatua changamoto za watoa huduma na watumiaji wa umeme, bidhaa za petroli, gesi asilia na maji na usafi wa mazingira.

Mha Mramba ameipongeza EWURA kwa hatua hiyo katika utoaji wa huduma bora kwa wananchi.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad