Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA) imeendelea kutoa elimu kwa Umma kwenye Maonesho ya Kimataifa ya Biashara ya 47 yanayofanyika katika Viwanja vya Sabasaba jijini Dar es Es Salaam na kuonesha huduma mbalimbali zinazotolewa na Bodi kwa wananchi waliofika kwenye Banda la Bodi hiyo lililopo ndani ya jengo la Wizara ya Fedha na Mipango.
Baadhi ya huduma zinazotolewa na NBAA katika kipindi hiki cha Sabasaba ni Usajili wa Wanafunzi ili kuweza kufanya mitihani ya Bodi hiyo kwa ngazi mbalimbali kuanzia ngazi ya chini (Accounting Technician) mpaka ile ya Taaluma (Profession) pamoja na usajili wa wanachama na makampuni ya kihasibu na Kikaguzi.
Pia NBAA wanatoa huduma zote ikiwemo jinsi ya kujisajili kufanya Mitihani, malipo ya Ada kwa Wanataaluma na wote wanaotaka kufanya usajili kwenye Bodi ya NBAA ni vizuri kufika katika Banda lao lililopo ndani ya Wizara ya Fedha na Mipango
Bodi hiyo kwa sasa inatumia mfumo wa kidijitari wa kutoa huduma zake hususan usajili wa wanafunzi na Wananchama kupitia tovuti yao, huduma hizo zinapatikana hata ukiwa sehemu mbalimbali pia kwa sasa huduma hizo zimehamia Sabasaba.
Afisa kutoka Bodi ya NBAA,Salim Kasumari (katikati) akitoa ufafanuzi kwa Samson Robert(kulia) kuhusu vituo vya kusomea kwa ajili ya kufanya mitihani ya Bodi alipotembelea Banda na Bodi hiyo kwenye Maonesho ya Kimataifa ya Biashara ya 47 kwenye Viwanja vya Sabasaba jijini Dar es Es Salaam. Kushoto ni Afisa kutoka Bodi ya NBAA, Eatella Mgaya
Afisa TEHAMA kutoka NBAA, Hassan Kawambwa (kushoto) akitoa maelezo kwa Asia Omary (kulia) kuhusu namna mtu anavyoweza kujisajili kupitia tovuti ya Bodi bila yeye kuja kwenye ofisi za Bodi alipotembelea Banda na Bodi hiyo kwenye Maonesho ya Kimataifa ya Biashara ya 47 kwenye Viwanja vya Sabasaba jijini Dar es Es Salaam. Katikati ni Afisa kutoka Bodi ya NBAA, Eatella Mgaya.
Bi Zawadi Msalla akisaini kitabu cha Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA) alipotembelea Banda la Bodi hiyo kwenye Maonesho ya Kimataifa ya Biashara ya 47 kwenye Viwanja vya Sabasaba jijini Dar es Es Salaam. Kulia ni Afisa kutoka Bodi ya NBAA, Eatella Mgaya na kushoto ni Afisa TEHAMA kutoka NBAA, Hassan Kawambwa.
CPA Makunga akitoa maoni yake kama mwanachama wa Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA) alipotembelea Banda la Bodi hiyo kwenye Maonesho ya Kimataifa ya Biashara ya 47 kwenye Viwanja vya Sabasaba jijini Dar es Es Salaam. Kulia ni Afisa kutoka Bodi ya NBAA, Eatella Mgaya na katikati ni Afisa TEHAMA kutoka NBAA, Hassan Kawambwa.
No comments:
Post a Comment