MFUKO wa Taifa wa Hifadhi ya
Jamii (NSSF) umewakaribisha wanachama na wadau kutembelea banda namba 13
wakati huu wa Maonesho ya 47 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam
kwenye viwanja vya Julius Nyerere maarufu Sabasaba, barabara ya Kilwa
jijini Dar es Salaam.
Maonesho hayo yameanza Juni 28 na yatafikia
kilele Julai 13, 2023 huku yakiwa yamebeba kaulia mbiu isemayo
"Tanzania Mahali Salama kwa Biashara na Uwekezaji".
Akizungumzia
Huduma ambazo mwanachama au mdau wa NSSF atazipata afikapo kwenye banda
hilo, Meneja Uhusiano na Elimu kwa Umma NSSF, Bi. Lulu Mengele alisema,
ni pamoja na kupata Elimu ya Hifadhi ya Jamii kwa Sekta Rasmi na Sekta
Isiyo Rasmi.
Pia alisema Mwanachama akifika kwenye banda hilo
ataweza kupata taarifa za michango yake ya kila mwezi lakini pia taarifa
za uwekezaji.
"Kuhusu taarifa za michango hii itamsaidi kujua
kama mwajiri wake anatekeleza wajibu wake wa kuwasilisha michango kwa
wakati au la na kama kuna changamoto zozote timu ya watumishi wa NSSF
iko tayari kuwahudumia." alifafanua Bi. Lulu Mengele.
Alisema Huduma nyingine ambayo Mwanachama atapata ni pamoja na kupata taarifa za Mafao yatolewayo na Mfuko.
Lakini pia kwa wananchi watakaotembelea banda hilo watapata taarifa za fursa za kujipatia viwanja na nyumba.
"Kama
mjuavyo NSSF tunauza viwanja, tunauza nyumba tungependa kuwakaribisha
wanachama wetu na wadau mbalimbali kutembela banda letu ili kuchangamkia
fursa hizo.” alisema.
No comments:
Post a Comment