FAIDA NNE ZA MKATABA KATI YA SERIKALI NA KAMPUNI YA DP WORLD - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Sunday, July 2, 2023

FAIDA NNE ZA MKATABA KATI YA SERIKALI NA KAMPUNI YA DP WORLD

 FAIDA #1 YA DP WORLD

Uwekezaji wa DP World kwenye bandari ya Dar es Salaam unatarajiwa kuongeza mapato ya serikali kutoka kwenye kodi ya forodha kwa asilimia 244, kutoka Shilingi trilioni 7.76 kwa mwaka 2021/22 hadi kufikia SHILINGI TRILIONI 26.7 kwa mwaka ifikapo 2032/33


FAIDA #2 YA DP WORLD
Uwekezaji wa DP World unatarajiwa kuongeza shehena inayohudumiwa na bandari ya Dar es Salaam kutoka tani milioni 18.4 kwa mwaka 2021/22 hadi kufikia tani MILIONI 47.5 kwa mwaka ifikapo 2032/33


FAIDA #3 YA DP WORLD
Iwapo DP World watafanya uwekezaji Tanzania, wataongeza meli zinazotia nanga kwenye bandari ya Dar es Salaam mara dufu kutoka meli 1,569 kwa mwaka kwa sasa, hadi kufikia MELI 2,950 kwa mwaka 2032/33

*Ongezeko hilo la meli litaongeza shehena za mizigo kwa wasafirishaji, ajira kwa Watanzania na mapato kwa Serikali.




FAIDA #4 YA DP WORLD
Uwekezaji wa DP World kwenye bandari ya Dar es Salaam unatarajiwa kuongeza ajira zinazotokana na shughuli za bandari kutoka ajira 28,990 kwa mwaka 2021/22 hadi kufikia AJIRA 71,907 ifikapo mwaka 2032/33. Hii ni sawa na ongezeko la mara 3 ya ajira zilizopo sasa hivi kwenye bandari ya Dar es Salaam


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad