Makamu wa Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa dkt Philip Mpango akiwa
katika picha ya pamoja na wanafunzi wa shule ya msingi Muyama mara baada
ya gafla ya kupokea vyumba vitatu vya madarasani ofisi mbili za walimu
na Samani mbalimbali za maofisini yaliokabidhiwa na Tanzania commercial
Bank (TCB), katika Shule ya Msingi Muyama iliyopo Wilaya ya Buhigwe
mkoani Kigoma.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango (wapili kulia), akikata utepe kuashiria
kupokea Madarasa, Samani mbalimbali na Ofisi za Walimu yaliokarabatiwa
na Tanzania Commercial Bank (TCB) katika Shule ya Msingi Muyama iliopo
Wilaya ya Buhigwe mkoani Kigoma ikiwa ni utaratibu wa Benki hiyo
kurudisha kwa kutoa msaada kwa jamii (CSR).
Hafla
hiyo imefanyika katika shule hiyo hivi karibuni wengine pichani ni
kutoka (kushoto), Afisa Mtendaji Mkuu wa Tanzania Commercial Bank,
Sabasaba Moshingi, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana,
Ajira na Wenye Ulemavu) Prof Joyce Ndalichako na viongozi wengine wa
serikalini pamoja na Maafisa wa Benki
MAKAMU wa Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania, Dkt Philip Mpango, ameishukuru Tanzania
Commercial Bank kwa kutoa msaada wa ukarabati wa Vyumba Vitatu vya
Madarasa, Ofisi Mbili za Walimu madawati 50 pamoja na printer na vitu
mbalimbali vya ofisini katika Shule ya Msingi Muyama iliopo Wilaya ya
Buhigwe mkoani Kigoma
Akipokea msaada huo aliushukuru ongozi
mzima wa Benki ya TCB kwa kuendelea kusaidia jamii katika suala zima la
Elimu Mkoa wa Kigoma na maeneo mengine hapa nchini.
Makamu wa
Rais Philip Mpango alipokea msaada huo alipokuwa kwenye ziara yake ya
kikazi mkoani humo na kutaka taasisi nyengine kuiga mfano mzuri
unaofanywa na Tanzania commercial bank
Ameeleza kuwa Benk ya TCB
imeonesha ukomavu wake hasa kwenye swala la elimu ya kifedha maana bila
elimu hakuna chochote kwenye maendeleo ya nchi yetu.
Dkt Mpango
ameongeza kuwa hata yeye amesoma katika shule hiyo ambayo leo Tanzania
commercial bank wametoa msaada wa vitu hivi kwaajili ya kukuza elimu na
maeneo mengine alisema mpango.
Nae Afisa Mtendaji Mkuu wa TCB, Bw
Sabasaba Moshingi alitoa shukrani za dhati kwa Mhe Mpango kwa kuweza
kufika kwenye hafla fupi ya makabidhiano na kuhaidi kuwa benki
itaendelea kusaidia jamii katika sekta mbalimbali ikiwemo elimu. Vile
vile alitoa rai kwa wananchi wa Buhigwe na maeneo ya karibu kuweza
kujiunga na huduma mbalimbali zinazotolewa na benki.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt Philip Mpango akiwa katika picha ya pamoja na maafisa kutoka benki ya TCB mara baada ya hafla ya kupokea vyumba vitatu vya madarasa na ofisi mbili za walimu na Samani mbalimbali za maofisini yaliokabidhiwa na Tanzania commercial Bank (TCB), katika Shule ya Msingi Muyama iliyopo Wilaya ya Buhigwe mkoani Kigoma.
No comments:
Post a Comment