UTEUZI HADHI YA BALOZI - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, June 13, 2023

UTEUZI HADHI YA BALOZI

 


 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi wa Viongozi wafuatao kuwa na Hadhi ya Balozi kama ifuatavyo:-


  1. Dkt. Moses Mpogole Kusiluka, Katibu Mkuu Kiongozi kuwa Balozi;


  1. Dkt. Salim Othman Hamad, Msaidizi wa Rais anayeshughulikia masuala ya Siasa kuwa Balozi; na 


  1. Dkt. Kassim Mohamed Khamis, Msaidizi wa Rais anayeshughulikia masuala ya Hotuba kuwa Balozi.


Uteuzi huu wa Hadhi ya Balozi umeanza tarehe 12 Juni, 2023.  


Aidha, Vyeo walivyonavyo vinabaki kama vilivyo.


Wateule wataapishwa tarehe 16 Juni, 2023 kuanzia saa 04:00 asubuhi - Ikulu, Chamwino - Dodoma


Zuhura Yunus
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad