HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, June 5, 2023

TUNAREJESHA UOTO WA ASILI KWA KUGAWA MICHE YA MITI BURE KWA WANANCHI, TAASISI MKOANI GEITA-TFS

 


Na Said Mwishehe, Michuzi TV-Geita

WAKALA wa Huduma za Misitu Tanzania(TFS)Mkoa wa Geita umesema kupitia kitalu cha miche ya miti Usindakwe ambacho ndio kitalu kikuu mkoani hapa kimekuwa kikiotesha miti na kisha kugawa bure kwa wananchi na taasisi ili kupanda katika mashamba yao lengo la kuendelea kurejesha uoto wa asili uliopotea kutokana na uharibifu wa mazingira.

Akizungumza na waandishi wa habari ,Msimakizi wa kitalu cha Usindakwe mkoani Geita ambaye pia ni Mhifadhi Misitu Sandusy Ngunyale amesema kitalu hicho kilichoanzishwa mwaka 2028 kimekuwa kinatumika kama kitalu kikuu na miche inayozalishwa inagawaiwa bure kwa wananchi wote wa mkoa huo kupitia utaratibu maalumu uliowekwa na mahitaji yamekuwa ni makubwa.

“Lengo la TFS kuanzisha kitalu hiki kikuu kwa Mkoa wa Geita ilikuwa ni kusaidia jamii ipate miti ya kupanda katika mashamba yao ili kujiongeza kipato na wakati huo huo kurejesha uoto wa asili ambao ulishapotea kutokana na ukataji miti uliokuwa umekithiri katika mkoa mzima wa Geita

“Tunazalisha miti hapa na tunaigawa kwa wananchi wa mkoa wetu wote wa Geiga, na kitalu chetu kina uwezo wa kuzalisha mpaka miche milioni moja lakini kwa sasa tunayo miche 300,000 na malengo yetu hadi mwishoni mwa mwaka wa fedha unaoanza 2023/2024 tuwe tuwe na miche 500,000,”amesema.

Amefafanua miche yote inayozalishwa inagaiwa bure kwa wananchi pamoja na taasisi zote zilizopo mkoani Geita , hivyo miche inapokuwa tayari TFS wanatangaza na kisha waombaji wawe wananchi au taasisi wanaandika barua ya kuomba miche.

“Tukishapa maombi kwa barua tunakwenda kuhakiki eneo analokwenda kupanda, tunampa miche lakini baada ya kupanda tunafuatilia kwa miezi kadhaa kuona kama miche inaendelea vizuri na kama kuna changamoto basi tunafuatilia kujua inatokana nini.”

Kuhusu mwitikio wa wananchi kuchua miti na kwenda kupanda ,amesema uko vizuri kwani msimu uliopita walikuwa na miche 300,000 na yote waliigawa haukubaki hata mche mmoja.

Hata hivyo amesema mbali ya kuotesha miti na kugawa kwa wananchi, kupitia kitalu hicho wananchi wamekuwa wakinufaika na ajira za muda ambazo zinatokana na kuhudumia kitalu hicho hivyo wamekuwa wakipata fedha za kuendesha maisha yao.

Kwa upande wake Mkazi wa Geita Majira Mussa akizungumza kwa niaba ya wananchi wa Mkoa wa Geita amesema wanaishukuru Serikali kwa kuanzisha kitalu hicho kwasababu kinawasaidia katika kuifanya Geita kuwa ya kijani kwani miti wanapewa bure.

“Miti inapokuwa tayari katika kitalu hiki tunachukua na kwenda kupanda katika shamba au eneo lako.Uwepo wa kitalu hiki umetunufaisha wananchi wengi wa Geita na kwa upande wangu binafsi ninafuka kwasababu kuna miti ya mbao na matunda, hivyo ninapohitaji mbao au matunda napata kwa urahisi.

“Pia kupitia kitalu hiki nimepata ajira ya kutunza bustani , hivyo napata kipato na kurahisha maisha yangu,”amesema huku akishauri wananchi kujitahidi kutunza mazingira ,wasiharibu misitu kwa fujo na watumie kitalu hicho kuendeleza uoto wa asili mkoani Geita.

Sehemu ya kitalu cha miche ya miti ikiendelea kutunzwa kitalu cha miti Usindakwe kilichopo mkoani Geita.Kitalu hicho    kinasimamiwa na Serikali kupitia Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania(TFS)
Mkazi wa Geita Mjini Majira Mussa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu faida za kitalu cha miche ya miti Usindakwe mkoani Geita

Sehemu ya kitalu cha miche ya miti ikiendelea kutunzwa kitalu cha miti Usindakwe kilichopo mkoani Geita.Kitalu hicho    kinasimamiwa na Serikali kupitia Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania(TFS)
No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad