Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) Abdul-Razaq Badru akizungumza na waajiri wa Sekta Binafsi wa Mkoa wa Dar es Salaam wanaofanya vizuri katika kukata asilimia 15 ya wafanyakazi katika hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
Picha ya pamoja ya waajiri wakiwa ngao ya kutambuliwa juu ya utekelezaji wa Sheria ya HESLB ya kukata asilimia 15 ya Mshahara ya wafanyakazi walionufaika HESLB.
Baadhi ya waajiri wakifatilia mada kwenye hafla ya kutambua waajiri bora kwa mkoa wa Dar es Salaam kwa kutekeleza sheria HESLB.
Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) Abdul-Razaq Badru akikabidhi ngao ya kutambua waajiri wa Sekta Binafsi wa Mkoa wa Dar es Salaam kwa Taasisi ya Afya ya Ifakara kwa kufanya vizuri katika kukata asilimia 15 ya mshahara kwa wafanyakazi walionufaika na HESLB katika hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mktendaji wa Taasisi ya Afya ya Ifakara Dkt. Honorati Masanja Akizungumza katika hafla hiyo wa niaba ya waajiri kuhusiana na utekelezaji wa matakwa ya kisheria ya kukata asilimia 15 ya mshahara kwa wafanyakazi walionufaika na mkopo kutoka HESLB.
Na Chalia Kibuda, Michuzi Michuzi TV
BODI ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu nchini (HESLB) leo (Jumatatu, Juni 5, 2023) imewatambua na kuwapa tuzo maalum waajiri 10 kutoka Mkoa wa Dar es Salaam kutokana na kuwasilisha kwa wakati makato ya wafanyakazi wao waliokopeshwa mikopo ya elimu ya juu kutoa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB).
Akizungumza katika hafla fupi ya kuwakabidhi ngao, Mkurugenzi Mtendaji wa HESLB, Abdul-Razaq Badru, amesema waajiri hao wamekuwa mfano kwani wamekuwa wakikata kwa wakati fedha za wafanyakazi wao kiasi cha asilimia 15 ya mshahara na kuwasilisha HESLB kupitia Mfumo wa Ki-elektroniki wa Malipo ya Serikali (GePG) katika hafla hiyo iliyofanyika katika ofisi za HESLB jijini Dar es Salaam.
“Tunathamini sana ushirikiano tunaopata kutoka kwa waajiri na ndiyo sababu tumeamua kuwatambua waajiri hawa kutoka sekta binafsi ili kuwahamasisha waajiri wengine ambao utekelezaji wao wa masharti ya Sheria ya HESLB hauridhishi kama inavyotarajiwa,” amesema Badru
Amesema Mkoa wa Dar es salaam ni mkoa pekee kati ya Julai 2022 hadi Mei 2023 tumekusanya Sh.Bilioni 17 kutoka sekta binafsi ambayo ni sawa na asilimia 22.3 ya jumla ya ya Sh.Bilioni 76 tulizokusanya kwa mwaka kutoka sekta binafsi nchini kote hivyo tunawashukuru kwa kuendelea kutuunga mkono.
Badru na amefafanua kuwa wataendelea kuwatambua waajiri katika mikoa mingine katika kuwatambua waajiri wa sekta bunafsi kwenye kukidhi matakwa ya sheria kwa wale walionufaika na mikopo waweze kurejesha.
Akizungumza katika hafla hiyo, Meneja wa HESLB Kanda ya Dar es salaam Anna Sabuni amewataja waajiri hao bora zaidi kwa mkoa wa Dar es salaam ni Benki ya Taifa ya Biashara (NBC); Benki ya Diamond Trust; Kampuni ya Coca Cola Kwanza; na Shule za Feza.
Waajiri wengine ni Kampuni ya Bia Serengeti; Kampuni ya SICPA Tanzania; Taasisi ya Kifedha ya Brac Ltd; Taasisi ya Afya Ifakara (IHI); Kampuni ya Simu ya Viettel (Halotel) Tanzania; na Shirika la GIZ.
“Ofisi yetu ya Kanda ya Dar es salaam ilianzishwa mwezi Novemba 2021 na hadi Juni 2022, tuliweza kukusanya TZS 12 bilioni kutoka kwa waajiri wa sekta binafsi na tumeona tunaweza kukusanya zaidi tukiendeleza ushirikiano,” amesema Anna Sabuni.
Akizungumza katika hafla hiyo wa niaba ya waajiri, Mkurugenzi Mktendaji wa Taasisi ya Afya ya Ifakara Dkt. Honorati Masanja aimeshukuru HESLB kwa kuandaa hafla hiyo na kushauri HESLB kuandaa mikakati ya kuwafikia waajiri wasiotii masharti ya sheria ili kuwaelimisha.
“Sisi tuilioalikwa tunatii na kutekeleza masharti ya sheria ya HESLB … sasa ni vema utaratibu kama huu ukafanywa kwa waajiri wasiotimiza masharti ili wabadilike baada ya kuelimishwa,” amesema Dkt. Masanja.
No comments:
Post a Comment