SEMINA YA WAPIGA PICHA NA VIDEO YAJADILI NAMNA YA KUTANUA MASOKO YA KIBIASHARA - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, June 7, 2023

SEMINA YA WAPIGA PICHA NA VIDEO YAJADILI NAMNA YA KUTANUA MASOKO YA KIBIASHARA

 JUKWAA la wanatasnia katika Fani ya upigaji picha na video wajadiliana namna ya kutafuta Masoko ya Kibiashara pamoja na kuunda umoja ambao utasaidia kupatiwa fursa mbalimbali za kutanua masoko ya Kibiashara.


Akizungumza na Wanahabari Mbezi Garden Hotel Jijini Dar es salaam mara baada ya Kumalizika kwa kongamano la Kwanza lililoandaliwa na Mratibu Rajab Mchatta kutoka Kampuni ya Big Solutions amesema Kwa mara ya Kwanza kumekuwa na muitikio mzuri hivyo kila mwaka kutakuwa na Kongamano hilo lenye lengo la kukamata fursa za kiuchumi.

"Madhumuni ya Semina hii ilikua ni kuwakutanisha wapiga picha na video wawe na Jukwaa lao ili waweze kubadilishana uzoefu na kujadili namna ambavyo wataweza kufanya kazi kwa ufanisi wakiwa na umoja wao ili serikali iweze kuwasaidia kupitia umoja huo i waweze kutanua Masoko yao ya Kibiashara. "


"Mnapokuwa pamoja mnakuwa na nguvu na ushawishi na kupata fursa na kujitathimini kwa kile mnachokifanya katika jamii hivyo semina hii imetengeneza umoja ,kubadilishana uzoefu ,kukutanisha watu mbalimbali ambao ni wabobezi katika tasnia hiyo."

Aidha ,Mchata ameongeza kuwa Semina itakuwa ikifanyika kila mwaka kwa lengo la kutathimini vitu mbalimbali ikiwemo fursa za kibiashara na kutafuta Masoko.


Kwa upande wake Meneja Masoko wa Benki ya Akiba Emmanuel Ishengoma amesema Watu wa Tasnia hiyo ni wajasiriamali hivyo benki hiyo inawajali wajasiriamali katika biashara zao na kuhaidikushirikiana nao bega kwa bega.

"Tunajua vifaa vinavyotumika ni vyenye thamani hivyo tunawakaribisha wafike ofisi za benki ya Akiba ili waweze kupata nafasi ya kukopeshwa fedha kwa ajili ya kuongeza ubora kwenye kazi zao,kupatiwa bima kwa ajili ya kulinda vifaa hivyo."

Nae mnufaika wa Semina hiyo Adel Alex ameeleza Mbali na kuongeza weledi, watoa mada wamegusia vitu mbalimbali ikiwemo maswala ya bima,uwekezaji, usalama kazini.

"Fursa ya kujifunza hivyo tunahaidi kuongeza weledi ili kuleta ufanisi katika kazi zetu na kukuza Masoko."

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad