OLAKIRA AFYATUA KOMBOLA MBILI ZENYE UJAZO - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, June 30, 2023

OLAKIRA AFYATUA KOMBOLA MBILI ZENYE UJAZOSTAA wa Afrobeat Olakira kutoka Nigeria, amesema hapoi wala haboi Kwa kuwapa radha ya ngoma mbili tamu mashabiki wake. Ngoma hizo ni "Ileke" na "Kisses,".

Olakira anasema ngoma hizi zimekuja kukata kiu kwani zitawafurahisha watu wate kwani zimwaukwa na kupewa midundo isiyozuilika. "Ileke," ni wimbo wangu wa kwanza kwenye hizi mbili ambao unamchanganyiko wa Afrobeat na sauti za kisasa, wimbo huu umetayarishwa na Simba Tagz, "Ileke." inamaana ya umaridadi, kujiamini, na fahari ya kitamaduni. Kwa upande mwingine, "Kisses" nimetayarisha mwenyewe, wimbo huu wa kusisimua unaangazia kina cha mapenzi na matamanio, ni wimbo wa mapenzi unaovutia ambao bila shaka utawaacha wasikilizaji kutamani zaidi, amesema msanii huyo.

Mwaka 2020 Olakira alitamba na kufanya vizuri na wimbo wake wa 'In My Maserati', Olakira ameendelea kuachia nyimbo nyingi zinazosifika sana na EP, pia akiwa msanii wa kwanza wa Kiafrika katika historia ya ulimwengu, kupata mikataba na kampuni maarufu ya magari ya kifahari ya Italia.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad