LSF Wazindua Jezi, kusaidia hedhi salama kwa wasichana - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, June 22, 2023

LSF Wazindua Jezi, kusaidia hedhi salama kwa wasichana

Legal Services Facility (LSF) na Smile for Community (S4C) ambao ni waratibu na waandaaji wa 'Run for Binti Marathon 2023'  wakiwa na wadau mbalimbali wakati wa uzinduzi wa jezi mpya zitakazotumika katika mbio hizo.
Meneja Rasilimali na Mawasiliano wa Legal Services Facility (LSF), Jane Matinde (kushoto) na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Smile for Community (S4C), Flora Njelekela wakionyesha jezi za 'Run for Binti Marathon 2023' zitakazofanyika tarehe 30 Julai 2023 Jijini Dar es Saalaam mara baada ya uzinduzi uliofanyika leo.Mkurugenzi wa Smile for Community (S4C), Flora Njelekela akizungumza na waandishi wa habari wakati wa kutangaza tarehe mpya ya mbio na kuzindua jezi zitakazotumiwa na wakimbiaji wa mbio za 'Run for Binti Marathon 2023' zitakazofanyika 30 Julai 2023 Jijini Dar es Salaam kwa lengo la kukusanya rasilimali fedha kuwezesha watoto wa kike Mkoani Lindi kupata bidhaa za hedhi salama.


JEZI zitakazotumika katika mbio za kuchangisha fedha za kusaidia watoto wa kike kuwa na mazingira bora ya kupata hedhi salama, zimezinduliwa leo Juni 22, 2023.

Jezi hizo zimezinduliwa na Shirika la Legal Services Facility (LSF), kwa kushirikiana na Shirika la Smile for Community (S4C), jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi Mkuu wa S4C, Flora Njelekela, amesewashukuru wadau wanaondelea kujitoa kwa ajili ya kufanikisha mbio hizo.

Naye Meneja wa Rasilimali na Mawasiliano kutoka LSF, Jane Matinde, amesema “naomba tujumike pamoja kama jamii na tuhamasishe wengine na tuonyeshe nguvu ya pamoja katika kujitolea. 

“Kwa michango yenu tunaweza kuleta matokeo chanya kwa mustakabali wa watoto wa kike nchini.  Tukielekea tarehe 30 Julai 2023 nawaomba wadau wote kushiriki mbio hizi kwa ajili ya kumuinua mtoto wa kike,” amesema.

Mbio hizo zinatarajiwa kufanyika tarehe 30 Julai 2023, ambazo zitahusisha washiriki zaidi ya 1,500, ambao watakimbia kwa lengo la kukusanya rasilimali fedha kwa ajili ya kuwezesha watoto wa kike kupata taulo ili kuboresha haki ya afya ya uzazi hususan hedhi salama.

Pia, zitasaidia kuboresha mazingira ya sekta ya elimu kwa mtoto wa kike yatakayomuwezesha kupata hedhi salama, kupitia ujenzi wa miundombinu hususan vyoo.

Sambamba na hilo vikundi vya wanawake vya kiuchumi katika ngazi ya jamii vitawezesha kwa kupatiwa mashine na vitambaa maalumu vitakavyowawezesha kushona sodo (taulo za kike) na kuziuza kwa bei nafuu kwenye shule mbalimbali na hivyo  kujiinua kichumi.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad