BONANZA LA AFYA NI MUHIMU KUJENGA AFYA ZA VIJANA. - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, June 16, 2023

BONANZA LA AFYA NI MUHIMU KUJENGA AFYA ZA VIJANA.

Na.Elimu ya Afya kwa Umma .

Afisa Maendeleo Halmashauri ya Jiji la Dodoma Daniel Mfungo Manyama amesema Bonanza la Afya katika mkoa wa Dodoma lililoandaliwa na Wizara ya Afya  lina umuhimu mkubwa kwa ajili ya vijana kutambua afya zao.

Manyama amesema hayo katika mwendelezo wa mashindano ya Bonanza hilo yaliyofanyika kata ya Kikuyu Kaskazini ambapo pia huduma mbalimbali za afya zimekuwa zikitolewa bure ikiwemo kupima afya, elimu ya lishe,afya ya uzazi kwa vijana.

“Bonanza hili ni muhimu kwa ajili ya vijana kutambua afya zao, tunaishukuru Wizara ya Afya kwa kuleta bonanza hili ,watu hasa vijana tunahimiza sana vijana kushiriki katika mabonanza kama haya kwani kuna huduma mbalimbali muhimu za afya zinatolewa pia elimu ya afya”amesema Manyama.

Katika mpira wa miguu kata ya Kikuyu Kaskazini timu za mpria wa miguu zilizoshiriki kwa mechi ya kwanza kulikuwa na timu ya  Enjoy Soccer dhidi ya Star Lion ambapo Enjoy Soccer waliibuka kuwa washindi kwa bao moja (1) kwa nunge(0), mechi ya pili ilikuwa dhidi ya  Malundoni FC na Star Lion ambapo Malundoni FC waliibuka Kidedea kwa goli  moja(1) kwa sifuri(0) huku mechi ya tatu ikichezwa dhidi ya Enjoy Star na Malundoni FC ambapo Malundoni FC pia iliibuka kuwa mshindi kwa kufunga bao  moja(1) kwa nunge(0).

Hivyo, kwa matokeo hayo timu ya Malundoni FC imetinga nusu fainali kwa siku ya Ijumaa Juni 16,2023 itapambana na timu ya  Gwasa kutoka kata ya Chang’ombe ambapo mchezo huo utachezwa katika Uwanja wa Mpira Chuo Kikuu cha St.John.

Ikumbukwe kuwa katika Afya Bonanza kata ya Kikuyu Kaskazini  watu 103  wamepata elimu na kupima masuala ya lishe  ambapo asilimia 12.6% wakibainika na utapiamlo, watu 80 wakipata elimu juu ya Magonjwa yasiyo ya kuambukiza ,watu 50  wamepima  Virusi vya UKIMWI(VVU), watu 44  wakipata elimu kuhusu masuala ya ukatili ambapo pamebainika kesi ya ulawiti wa mtoto mwenye umri wa miaka mitano na watu watano wakibainika na matatizo ya magonjwa ya akili.


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad