HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, May 22, 2023

THRAPA WAADHIMISHA SIKU YA 'HR' BILA BODI, WAASWA KUUNDA BODI ITAYOSHUGHULIKIA MASLAHI YAO

 

Wazungumshi wakuu akizungumza wakiwa kwenye mkutano mkuu wa Wataalamu wa Rasilimali watu na Utawala wa mwaka uliofanyika katika kituo Cha Mikutano cha Julius Nyerere (JINCC) mwishoni mwa wiki.

CHAMA Cha wataalaamu wa Rasilimali watu (HR) na Utawala  (Administration) (THRAPA) waadhimisha siku ya Rasilimali watu ambayo hufanyika kila mwaka ifikapo Mei 20 wakiwa hawana bodi ya kusimamia Masuala yao.


Hayo ameyasema Mbunge wa jimbo la Kilwa Kusini, Ally Kasinge wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam wakati wa kufunga mkutano mkuu wa mwaka uliofanyika jijini Dar es Salaam katika kituo Cha Mikutano cha Julius Nyerere (JINCC) amesema sasa kuna haja kuunda bodi ambayo itakuwa ikishughulikia masuala mbalimbali yanayohusiana na taaluma hizo.

Amesema kuwa THRAPA wanatakiwa kutokuwa na mgongano kati ya taaluma ya Rasilimali watu na taaluma ya utawala kwani taaluma hizo zote zinasimamia bali moja inashimamia rasilimali watu na Utawala inasimamia Rasilimali zingine kama fedha.

"Kumekuwa kama na Mgongano wa kimaslahi, kwahiyo kupitia mkutano huu kunahaja ya kuunganisha taaluma hizi mbili kwani wote ni wasimamizi." Amesema Kasinge

Akizungumzia kuhusiana na maslahi ya taaluma hizo mbili amesema kuwa kusiwepo na utofauti katika maslahi kati ya HR na Administration wawe wanawiana kimaslahi kwa sababu wote taaluma zao zinafanana.

Pia amewaasa kujitambua kama wanataaluma kwani wanamajukumu ya kusimamia rasilimali za taasisi au kampuni katika maeneo yao ya kazi.

Awali wakati akimkaribisha mgeni rasmi Mwenyekiti wa THRAPA, Gerald Ruzika amesema kuwa mkutano huo umejumuisha wataalamu wa kada zote mbili ambazo zilikuwa hazitambuliki sasa taaluma hizi zitakuwa zikitambulika kwani watakuwa wanakutana kila mwaka ili jamii ijue kuwa taaluma hiyo ipo.

"Kada hii kwa kiasi flani imekuwa haitambuliki, sasa tunataka nchi hii ijue kubwa zaidi ni hii ya la kutokutambulika, lakini wakati mwingine watu kudhani kwamba kazi hii inaweza ikafanywa na mtu yeyote sio kila mtu anaweza kuteuliwa akafanya kazi hizi". Amesema Ruzika

Amesema kuwa kama taasisi itakuwa haina rasilimali watu inayofanya kazi katika taasisis basi lazima mambo yaende kombo.
Mbunge wa jimbo la Kilwa Kusini, Ally Kasinge akizungumza jijini Dar es Salaam wakati wa kufunga mkutano mkuu wa mwaka uliofanyika katika kituo Cha Mikutano cha Julius Nyerere (JINCC) mwishoni mwa wiki.
Mwenyekiti wa THRAPA, Gerald Ruzika akizungumza jijini Dar es Salaam wakati wa kufunga mkutano mkuu wa mwaka  wa Wataalamu wa Rasilimali watu na Utawala uliofanyika katika kituo Cha Mikutano cha Julius Nyerere (JINCC) mwishoni mwa wiki.
Matukio mbalimbali ya Wataalamu wa Rasilimali watu na Utawala wakati wa kufunga mkutano mkuu wa mwaka uliofanyika katika kituo Cha Mikutano cha Julius Nyerere (JINCC) mwishoni mwa wiki.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad