RUSHWA INAKWAMISHA MAENDELEO NA HUDUMA NDANI YA JAMII,:;" WANAOJIHUSISHA NA RUSHWA WAFICHULIWE -KAIM - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Sunday, May 21, 2023

RUSHWA INAKWAMISHA MAENDELEO NA HUDUMA NDANI YA JAMII,:;" WANAOJIHUSISHA NA RUSHWA WAFICHULIWE -KAIM

 


Na Mwamvua Mwinyi, Kibiti
KIONGOZI wa mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa Mwaka huu Abdallah Shaib Kaim, ameeleza licha ya juhudi za Serikali kuboresha huduma na miradi mbalimbali ,wapo baadhi ya wala rushwa wanaokwamisha na kuzorotesha juhudi hizo.


Kutokana na hilo ametoa rai kwa Watanzania kushirikiana na Serikali kufichua wanaojihusisha na vitendo vya rushwa.


Akizindua mradi wa club ya mapambano dhidi ya rushwa kata ya Bungu kijiji cha Nyambili/Nyambunda, Shaib aliwaasa wananchi kuwa tayari kutoa ushahidi Mahakama endapo kuna taarifa za wala rushwa.


"Japo kuna kazi kubwa inafanywa na Serikali katika kuboresha huduma mbalimbali ,katika sekta ya afya,elimu," Tumetembelea miradi mingi na ya kimkakati lakini zipo sehemu kazi hiyo inakwamishwa na vitendo vya rushwa "alielezea Shaib.

Hata hivyo,Shaib alieleza kati ya jumbe maalum za Mwenge mwaka huu ,unalenga kutuelimisha mapambano dhidi ya rushwa, alitaka tutimize wajibu wetu dhidi ya mapambano ya vitendo vya kutoa na kupokea rushwa.


Sambamba na hilo,alikagua na kisha amejiridhisha kuzindua mradi wa madarasa matano shule ya Sekondari Nyambili/Nyambunda, kuzindua darasa na ofisi shule ya Msingi Roja.

Awali Mwenge wa Uhuru umepokelewa wilayani Kibiti ukitokea wilaya ya Rufiji ambapo ukiwa wilayani humo utapitia Miradi 15 yenye thamani ya Bilioni 1.3.

Mkuu wa wilaya ya Kibiti, Kanal Joseph Kolombo alieleza, kati ya miradi hiyo minne itazinduliwa, mitatu itafunguliwa ,jiwe la msingi miwili pamoja na mitano kukaguliwa kwenye umbali wa km.171.05.

Kolombo alisema, kati ya miradi hiyo pia Mwenge huo umefungua jengo la upasuaji kituo cha afya Kibiti na daraja la Mkelele lililopo kata ya Salale Kijiji cha Nyamisati na kukagua mradi wa Utunzaji Mazingira na uhifadhi wa vyanzo vya maji Salale.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad