HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, May 17, 2023

TANZANIA NA JICA KUSHIRIKIANA KATIKA KUJENGA UWEZO WA MATUMIZI BORA YA GESI ASILIA

 WIZARA ya Nishati pamoja Shirika la Kimataifa la Maendeleo la Japan (JICA) wamesaini makubaliano ya kutekeleza mradi wa kujengea uwezo Wataalam wa Wizara na Taasisi zake katika eneo la kuendeleza matumizi bora ya Gesi Asilia ili kuiwezesha Tanzania kuendelea kunufaika kiuchumi na rasilimali hiyo.


Makubaliano hayo yamesainiwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Mhandisi Felchesmi Mramba na Mwakilishi Mkuu wa JICA Tanzania, ARA Hitoshi tarehe 16 Mei, 2023 jijini Dar es Salaam.

Makubaliano hayo yatapelekea wataalam wa Tanzania kuongeza ufanisi katika kufanya mipango na kutekeleza miradi ya matumizi ya Gesi Asilia kwa kuzingatia pia suala la utunzaji wa mazingira.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Mhandisi Felchesmi Mramba (kushoto) na Mwakilishi Mkuu wa JICA Tanzania, ARA Hitoshi wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kusaini makubaliano ya kutekeleza mradi wa kujengea uwezo Wataalam wa Wizara ya Nishati na Taasisi zake katika eneo la kuendeleza matumizi bora ya Gesi Asilia.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad