HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, May 17, 2023

DART kujenga miundombinu majiji yanayokua kwa Kasi

 

Meneja wa Mipango Usafirishaji Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka (DART), Mhandisi Mohamed Kuganda akionesha mchoro wa barabara za Mabasi yaedayo haraka zilizojengwa na zitakazojengwa jijini Dar es Salaam wakati akiwasilisha mada kuhusu miundombinu ya DART katika semina ya kuwajengea uwezo waandishi wa habari zinazohusu DART inayofanyika kwenye hoteli ya Dodoma City jijini Dodoma.
Meneja wa Mipango Usafirishaji Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka (DART), Mhandisi Mohamed Kuganda akifafanua jambo kwa washiriki wa semina  wakati akiwasilisha mada kuhusu miundombinu ya DART katika semina ya kuwajengea uwezo waandishi wa habari zinazohusu DART inayofanyika kwenye hoteli ya Dodoma City jijini Dodoma.


Na Chalila Kibuda , Michuzi TV , Dodoma 

WAKALA wa Mabasi Yaendayo Haraka (DART) imesema  katika ukuaji wa miji na nchini wanatarajia kwenda kwenye miji mengine   kutengeneza miundombinu ya barabara ya mabasi yaendayo haraka.


Miji inayokuwa kwa kasi ni majiji ya Dodoma , Mwanza, , Mbeya, Arusha pamoja na Tanga ikiwa kurahisisha huduma ya usafiri katika kuchochea uchumi ya kusafiri sehemu moja kwenda nyingine.


Akizungumza Jijini Dodoma katika semina ya kuwajengea uwezo waandishi wa habari kuhusu utekelezaji wa miradi ya mabasi yaendayo haraka,  Meneja wa Mipango Usafirishaji Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka (DART), Mhandisi Mohamed Kuganda, amesema kuwa serikali inaendelea na juhudi kufikia Mikoa inayokuwa kwa kasi ili kufikisha huduma ya usafiri.

“Lengo la serikali na wadau  ni  kuhakikisha inatengeneza mifumo ya miundombinu ya mabasi yaendayo haraka Mikoa yote ili kuhakikisha tunaondoa changamoto ya usafiri” amesema Kuganda.

Hata hivyo amesema  wanaendelea na utekelezaji miradi katika Mkoa wa Dar es Salaam ambapo mradi huo una awamu sita.

Amesema kuwa utekelezaji wa awamu ya kwanza tayari umemalizika, kwa sasa wanaendelea na ujenzi wa awamu ya pili DART Mbagala ambapo umefikia asilimia 85.

“Mradi wa awamu ya tatu Gongo la Mboto tayari umeaza na umefika asilimia 10 katika utekelezaji wake” amesema.

Amesema kuwa awamu ya nne ni ujenzi kutoka Tegeta kwenda mjini huku awamu ya tano utejengwa Ubungo pamoja na awamu ya sita ni muendelezo wa mradi wa awamu kwanza na pili kutoka Mbagala Rangi Tatu hadi Vikindu, kutoka Kimara hadi Kibaha.

Kuganda amesema kuwa tayari fedha zote za utekelezaji wa miradi wa DART katika Mkoa wa Dar es Salaam zipo tayari lengo ni kuhakikisha malengo tarajiwa yanafikia.

Aidha amesema Wakala ya Mabasi Yaendayo Haraka (DART) ni taasisi ya serikali iliyoundwa kwa mujibu wa tangazo la serikali No. 120 la tarehe 25 Mei 2007 chini ya sheria No. 30 ya Wakala za Serikali ya mwaka 1997 na marekebisho yake.

Mhandisi Kuganda amesema lengo  kuu la DART ni kuanzisha na kuendesha mfumo wa Usafiri wa Mabasi Yaendayo Haraka kwa jiji la Dar es Salaam.

Miongoni mwa malengo ni kuhakikisha kuna mtiririko bora wa usafiri kwenye mitaa na barabara za mjini, usimamizi wa wakala wenye ufanisi.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad