HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, May 18, 2023

NBAA YATOA MSAADA WA VITABU KATIKA SHULE YA SEKONDARI YA MAKURUMLA


Mwenyekiti wa Bodi ya Shule ya Sekondari ya Makurumla Aristes Udindo akipokea vitabu vya masomo ya biashara na hesabu kutoka kwa Mfanyakazi wa Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA), Sawa Ngendabanka wakati wa bodi hiyo ilipotembelea katika shule hiyo na kutoa msaada wa vitabu vya masomo ya Biashara vipatavyo 300 ikiwa ni kurudisha kwa jamii ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 50 tangu kuanzishwa kwa NBAA pamoja na kuwahamasisha wanafunzi hao kujiunga na masomo ya uhasibu watakapomaliza masomo yao ya Sekondari.
Wafanyakazi wa Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA) wakiwa kwenye picha ya pamoja na Wajumbe wa Bodi ya Shule ya Sekondari ya Makurumla wakiongozwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Shule hiyo Aristes Udindo(katikati) mara baada ya Bodi ya NBAA kukabidhi vitabu 300 vya masomo ya Biashara ikiwa ni kurudisha kwa jamii ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 50 tangu kuanzishwa kwa NBAA pamoja na kuwahamasisha wanafunzi hao kujiunga na masomo ya uhasibu watakapomaliza masomo yao ya Sekondari. Wa pili kulia ni Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Makurumla Naomi Alimosa.
Mfanyakazi wa Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA), Sawa Ngendabanka akiwahamasisha wanafunzi hao kujiunga na masomo ya uhasibu watakapomaliza masomo yao ya Sekondari ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 50 tangu kuanzishwa kwa NBAA kwa wanafunzi wanaosoma masomo ya Biashara katika shule ya Shule ya Sekondari ya Makurumla iliyopo Manispaa ya Ubungo jijini Dar Es Salaam
Baadhi ya Wanafunzi wanaosoma masomo ya Biashara katika Shule ya Sekondari ya Makurumla wakifuatilia mafunzo yaliyokuwa yanatolewa na wafanyakazi wa Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA) walipotembelea shuleni hapo kwa ajili ya kutoa msaada wa vitabu vya masomo ya Biashara pamoja na kutoa elimu ya kazi zinazofanywa na bodi hiyo.
Baadhi ya vitabu vilivyotolewa na Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA) katika shule ya Sekondari ya Makurumla ikiwa ni kurudisha kwa jamii ikiwa ni sehemu ya mpango wa maadhimisho ya miaka 50 tangu kuanzishwa kwa Bodi hiyo.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad