Na.Vero Ignatus,Arusha
Mei 21,2023 Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi (NACTVET) wametangaza rasmi wamefungua dirisha la udahili kwa wanafunzi wanaotaka kujinga na vyuo mbali mbali hapa nchini katika mwaka wa masomo 2023/2024.
Akizungumza na waandishi wa habari Jijini Arusha Mkurugenzi wa udhibiti, ufuatiliaji na Tathimini NACTVET Dkt, Jofrey Oleke, amebainisha kwamba udahili huo wa kozi zote zinazotolewa na vyuo mbali mbali wamefungua rasmi hadi Juni 30, 2023 katika awamu ya kwanza.
Amesema kuwa wahitimu wote wa Elimu ya Sekondari na vyuo vyenye sifa za kujiunga na kozi za Astashahada na Stashahada, wanashauriwa kufanya maombi yao kwa umakini ili kupata nafasi ya kujiunga na kozi wanazo zipenda". Amesema Dkt Oleke.
Amesisistiza kuwa wanafunzi wote wawe wametimiza sifa na vigezo vya kujiunga na vyuo katika kozi walizo omba kwa mwaka wa masomo 2023/2024 na maombi hayo ya kujiunga yatumwe katika vyuo husika". Ameongeza Dkt, Oleke.
Sambamba na hayo Dkt, Oleke alielezea kuwa wanafunzi wanaotaka kujiunga na programu/ kozi za Afya na Sayansi Shirikishi kwa upande wa Tanzania Bara wanapaswa kuwasilisha maombi yao kupitia udahili wa pamoja .
Dkt, Oleke.wametoa mawasiliano kwa wanafunzi wanaopenda kujiunga na kupitia kozi ya Afya na Sayansi Shirikishi hawa wanapaswa kuwasilisha maombi yao kupitia udahili wa pamoja yaani Central Admission System _ CAS, katika tovuti ya Baraza www.nacte.go.tz". Amesema
No comments:
Post a Comment