HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, May 1, 2023

MCHUNGAJI MBOGO: NJIA PEKEE YA KUKABILIANA NA USHOGA NI MAADILI KWA JAMII NA MUNGU

 

Mchungaji wa Kanisa la Moravian Usharika wa Singida Mjini, Yona Mbogo, akiwaombea Wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Mwenge wanaotarajia kufanya mitihani yao ya mwisho hivi karibuni wakati akihubiri ibada ya Jumapili iliyofanyika leo Aprili 30, 2023 katika Kanisa Kuu la Moravian Singida liliopo eneo la Mwenge Manispaa ya Singida

Na Dotto Mwaibale, Singida
MCHUNGAJI wa Kanisa la Moravian Usharika wa Singida Mjini, Yona Mbogo amesema njia pekee ya kupambana na vitendo vya mmomonyoko wa maadili ukiwamo ushoga na usagaji ni kumtegemea Mungu lakini kuwakamata na kuwaweka gerezani wanaojihusisha na vitendo hivyo ni kuongeza ukubwa wa changamoto hiyo.

Mchungaji Mbogo ameyasema hayo wakati akihubiri ibada ya Jumapili iliyofanyika leo Aprili 30, 2023 katika Kanisa Kuu la Moravian Singida liliopo eneo la Mwenge Manispaa ya Singida ibada ambayo somo lake kubwa lilihusu umuhimu wa utoaji wa zaka .

"Jambo hili la mapenzi ya jinsia moja ni pana hivi mfano unapowakamata wanaojihusisha na vitendo hivyo unakwenda kuwaweka gereza gani kwasababu hivi vitendo vinafanywa kati ya mwanaume na mwanaume, mwanamke dhidi ya mwanamke," alihoji Mchungaji Mbogo.

Alisema kutokana na mazingira ya jambo hili yalivyo njia pekee inayoweza kusaidia kukabiliana na vitendo hivyo ni jamii kuendelea kuzingatia masuala ya maadili kuanzia ngazi za familia na kumtumainia Mungu atuepushe na janga hilo.

Alisema kuporomoka kwa uchumi wa kipato kwa jamii ndiko kumetoa mwanya kwa baadhi ya wafadhili kupenyeza fedha kupitia Taasisi zisizo za kiserikali (NG'OS) na watu binafsi ambazo zimekuwa zikitumika kuhamasisha vitendo hivyo.

Akizungumzia suala la utoaji wa sadaka na zaka alisema ni jambo kubwa katika imani kwani mtu anayemtolea Mungu zaka kwa ukamilifu umuongezea mara dufu tofauti na yule anayekuwa mwizi wa kumuibia zaka hiyo kwa kutoa chache tofauti na ile aliyojaliwa kama alivyofanya Anania na mke wake Safina waliotajwa katika biblia ambao walishindwa kutoa zaka yao kwa ukamilifu kutokana na udanganyifu.

Alisema Mungu amehimiza kutolewa zaka asilimia 10 kutoka mapato ya kila kitu kinachopatikana iwe mshahara, mazao, mifugo na vinginevyo.

Alisema mtu anapotoa zaka kwa uaminifu Mungu anatengeneza agano kati yake pamoja na kizazi chake chote akimtolea mfano Abrahamu jinsi alivyo barikiwa baada ya kutoa kwa unyenyekevu na uaminifu akawa tajiri mkubwa.

Aidha, Mchungaji Mbogo alisema kutoa zaka kwa Mungu isiyo kamili ina leta laana kwa vizazi hadi vizazi na kusabisha mtu kupata matokeo mabaya ya maisha yake ikiwemo mikosi kama kufukuzwa kazi, kufeli masomo, magonjwa, biashara kudorora, kupata fedha lakini zinapotea pasipo ya sababu kutokana na matumizi yasiyofahamika na mengine mengi yanayofanana na hayo hadi kufikia hatua akidhani amerogwa.

Alisema mtu akishindwa kutoa sadaka ya Sh.500 hata akipata Sh.Milioni 1 hata weza kutoa hivyo aliwaomba waumini wa kanisa hilo kujenga tabia ya kumtolea Mungu sadada na zaka na Mungu atawabariki na vizazi vyao.

Mchungaji Mbogo akizungumzia umuhimu wa kwenda kusali alisema kuna watu wamekuwa wakichelewa kwenda ibadani kwa kutoa visingizio mbalimbali vikiwemo sikuwa na nauli au mtoto alikuwa mgonjwa na vingine vingi lakini mtu huyo huyo anapokuwa na jambo lake la kupata fedha kama kwenda kwenye vikoba yupo tayari kukodi hadi bodaboda ili afike haraka.

"Jambo hili sio zuri na halimpendezi Mwenyezi Mungu nawaombeni wakristo kujenga tabia ya kuwahi kufika kanisani mapema tuacheni tabia ya kuwa na sababu mbalimbali" alisema Mchungaji Mbogo.



Katika ibada hiyo Mchungaji Mbogo alifanya maombi maalumu ya kuwaombea Wanafunzi wa Sekondari ya Mwenge ambao wanatarajia kufanya mitihani yao ya mwisho hivi karibuni.


Mchungaji Mbogo akisisitiza jambo kwenye ibada hiyo.
Waumini wa kanisa hilo wakiwa kwenye ibada hiyo.
Wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Mwenge wakiwa kwenye ibada hiyo.
Ibada ikiendelea.
Mchungaji Mbogo akiwapa mkono wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Mwenge akiwatakia mitihani mema baada ya kuwaombea.
Kwaya ya Moravian Singers Singida ikitoa burudani ya nyimbo za kumsifu Mungu wakati wa ibada hiyo.
Wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Mwenge wakitoa burudani ya nyimbo za kumtukuza Mungu kwenye ibada hiyo.
Waumini wa kanisa hilo wakiwa nje baada ya ibada kumalizika.
Wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Mwenge wakiwa nje ya kanisa hilo baada ya ibada kumalizika.
Muonekano wa Kanisa la Moravian Mkoa wa Singida.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad