Lodge
mpya ijulikanayo kama FK lodge imezinduliwa mkoani Tabora na Mwakilishi
wa Mstahiki Meya , Diwani wa Kata ya Ipuli, Mh Molo Juma Molo. Lodge
hiyo ya kisasa yenye vyumba 13 itaongeza upatikanaji wa malazi kwa
wageni wa ndani na nje ya nchi wanaotembelea Mkoani hapo kwa sababu
mbalimbali
Akiongea wakati wa Uzinduzi Mkurugenzi Mkuu wa FK
Lodge , Bwana Frederick Kanga amesema maono ya kuwekeza Tabora yameenda
sambamba na kukuwa kwa haraka kwa mkoa Tabora hususani kwenye miundo
mbinu ya Reli ya kisasa ambayo ikikamilika itaongeza mzunguko wa fedha
na shughuli mbalimbali za kiuchumi kipindi cha ujenzi na hata baada ya
reli kukamilika.
Kwa upande wake Mgeni Rasmi Mwakilishi wa Mstahiki Meya , Mh Molo Juma Molo Awapongeza sana wakurugenzi na wamiliki wa FK Lodge kwa kuwekeza Tabora na kuahidi kutoa ushirikiano katika kukuza na kuwepo kwa mazingira bora ya uendeshaji wa biashara na kutoa wito kwa wadau wengine hususani wawekezaji wa ndani kuwekeza katika Mkoa wa Tabora.
Akiongea huduma zinazopatikana Makamu Mkurugenzi wa FK Lodge , Bi Jane Matinde Kanga amesema lodge hii ina vyumba 13 vyenye huduma zote muhimu ikiwemo WiFi , lakini huduma za vyakula na vinywaji pia vinapatika katika lodge hii. Aliongeza kwa kusema”Tunajisikia fahari kuweza kutengeneza Ajira kwa vijana 9 zitakazowawezesha kujikwamua kiuchumi , kadhalika tumeingia mikataba makapuni mbalimbali ya kutoa huduma kama za broadband, ulinzi, maji , umeme na hivyo kuchangia katika ungezeko la mapato yao na hivyo kukuza uchumi na pato la taifa kupita kodi. Matumaini na maono yetu kuwa kuwepo kwa lodge hii ni mwanzo wa nyingine nyingi katika maeneo mbalimbali nchini”.
Kupata taarifa zaidi tembelea tovuti ya FK Lodge :
Mkurugenzi Mkuu wa FK Lodge , Bwana Frederick Kanga akiongea wakati wa uzinduzi wa FK lodge iliyopo Ipuli Tabora
Mgeni Rasmi Mwakilishi wa Mstahiki Meya , Diwani wa Kata ya Ipuli, Mh Molo Juma Molo na Mkurugenzi Mkuu wa FK Lodge , Bwana Frederick Kanga wakikata keki wakati wa uzinduzi wa FK Lodge Tabora
Wafanyakazi wa FK Lodge wakiwa katika picha ya pamoja na Makamu Mkurugenzi wa FK Lodge , Bi Jane Matinde Kanga wakati wa Uzinduzi wa Lodge hiyo
Wamiliki wa FK Lodge Bwana na Bibi Frederick Kanga wakiwa katika picha ya pamoja wakati wa uzinduzi wa lodge mkoani Tabora
Mgeni Rasmi Mwakilishi wa Mstahiki Meya , Diwani wa Kata ya Ipuli, Mh Molo Juma Molo akiangalia muonekano wa lodge ndani wakati wa uzinduzi wa lodge hiyo
Mgeni Rasmi Mwakilishi wa Mstahiki Meya , Diwani wa Kata ya Ipuli, Mh Molo Juma Molo akiangalia muonekano wa lodge ndani wakati wa uzinduzi wa lodge hiyo
Wadau wa FK Lodge Joe na Mikidadi wakifungua champaign wakati wa uzinduzi
Wageni waalikwa wakipata chakula cha pamoja wakati wa uzinduzi
Baadhi ya wafanyakazi wa Exim walihudhuria uzinduzi wa FK Lodge mkoani Tabora

No comments:
Post a Comment