HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, May 24, 2023

Kampeni ya Mama Samia yazinduliwa Mkoani Manyara, Mamia ya wananchi Wapewa huduma za Msaada wa Kisheria bure

 WASAIDIZI wa msaada wa kisheria kutoka wilaya zote mkoani manyara wanaofadhiliwa na Shirika la Legal Services Facility LSF, wameshiriki katika uzinduzi wa kampeni ya Mama Samia ya Msaada wa Kisheria katika mkoa wa Manyara na kutoa elimu na huduma za msaada wa kisheria kwa wananchi bure.


Kampeni hii ya Kitaifa ya Huduma ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia imelenga kulinda na kukuza upatikanaji wa haki kwa wote kupitia huduma ya msaada wa kisheria nchini na itadumu kwa muda wa miaka mitatu.

Malengo mahususi ya hii kampeni ni kuongeza uelewa wa kisheria na haki za binadamu kwa jamii hususani haki za wanawake na watoto, kuimarisha huduma ya ushauri wa kisheria na kutatua migogoro kwa wananchi na kuweka mazingira wezeshi ya upatikanaji wa huduma za kisheria na kufanya huduma hizi kuwa endelevu.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampeni hiyo ya kitaifa katika mkoa wa Manyara, Mkurugenzi wa Programu na Uendeshaji kutoka LSF, Amani Manyelezi amesema, Kampeni hii imeenda sambamba na kazi tunazozifanya kwa takribani miaka 11 za kuwezesha upatikanaji wa haki kwa wote kupitia watoa huduma zaidi ya 4,000 waliopewa mafunzo ya kisheria nchi nzima Tanzania bara na Zanzibar.

Aidha, Manyelezi ameongeza kuwa, Kwa mwaka tunawafikia watu million 7 kupitia elimu ya kisheria.

Vilevile tunapokea migogoro takribani 70,000 ambapo asilimia 60 inatatuliwa na wasaidizi wa kisheria na hivyo kupunguza msongamano mahakamani.

Kampeni hii ina tija kubwa kwetu kwani tumepanga kufikia maeneo, ambayo ni ngumu kufikiwa na huduma hizi, hivyo tumejipanga kushirikiana na Serikali kimalilifu katika kutekeleza na kufikia malengo yetu.

”Katika utekelezaji wa kampeni ya Mama Samia mkoani Manyara, huduma za msaada wakisheria zinatolewa katika viwanja vya Stendi ya zamani Manyara na itaendelea katika muda wa siku 10 mfululizo kwa wilaya zote za mkoa wa Manyara ikiwemo Babati, Hanang, Simanjiro, Mbulu TC, Mbulu DC na Kiteto, ambapo katika siku pekee ya ufunguzi wasaidizi wa kisheria wamepokea kesi 45 na kuzishughulikia.
Mkurugenzi wa Programu na Uendeshaji kutoka Legal Services Facility (LSF), Amani Manyelezi akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampeni ya kitaifa ya Mama Samia Mkoani Manyara.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad