HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, April 28, 2023

Waziri Mkuu awataka wananchi kutumia kampeni ya Samia Aid kutokomeza ukatili

 

Waziri Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa Majaliwa akizungumza na Wasaidizi wa kisheria kutoka wilaya ya zote za mkoa wa Dodoma mara baada ya kutembelea banda la LSF wakati wa tukio la uzinduzi wa 'Mama Samia Legal Aid Campaign' kwenye Mkoa wa Dodoma uliofanyika 27.04.2023

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa Majaliwa akiwa katika banda la LSF baada ya kutembelea ambapo alipata maelezo kutoka kwa Msaidizi wa Kisheria Mkoa wa Dodoma, Kapesa Mawazo, kuhusu maandalizi ya utekelezaji wa 'Mama Samia Legal Aid Campaign' ulioanza 28 Aprili 2023 katika wilaya na halmashauri nane zikiwemo Mpwapwa, Kondoa, Bahi, Dodoma DC,  Chamwino, Chemba, Dodoma Mjini na Kongwa. Wasadizi wa kisheria ndio watekelezaji wa kampeni hii muhimu katika ngazi za wilaya hapa nchini wakishirikiana na wadau wengine.

Pichani ni Meneja Rasilimali na Mawasiliano wa Legal Services Facility, Jane Matinde (mwenye shati jeupe) akifafanua jambo mbele ya Waziri Mkuu wa Tanzania wakati wa uzinduzi wa 'Mama Samia Legal Aid Campaign' Jijini Dodoma uliofanyika 27.04.2023
WAZIRI vitendo vya ukatili wa kijinsia vikiendelea kuripotiwa nchini Waziri Mkuu wa Tanzania Kassim Majaliwa, amewataka wananchi kutumia Huduma ya msaada wa kisheria ya Mama Samia (Samia Legal Aid Campaign), kitokomeza vitendo vya ukatili wa kijinsia.

Waziri Majaliwa ametoa wito huo Jana Alhamisi,wakati akizindua kampeni hiyo kwa Mkoa wa Dodoma, inayoanza Leo tarehe 28 Aprili 2023, katika halmashauri nane mkoani humo ikiwemo Mpwapwa, Kondoa, Bahi na Dodoma Mjini.

"Kampeni hii itasadia kuboresha upatikanaji wa Haki kwa watu wasiojiweza, hususan wanawake, watoto na makundi mengine yaliyo katika mazingira magumu. Vilevile itachangia kuimarisha amani na utulivu, kuongeza kipato na kuleta utengamano wa kitaifa," amesema Waziri Majaliwa.

Waziri Majaliwa amesema kampeni hiyo itasadia kuimarisha mfumo wa utoaji Huduma za msaada wa kisheria kuanzia Serikali Kuu Hadi Serikali za Mitaa.

Pia, Waziri Majaliwa ameiagiza Wizara ya Katiba na Sheria, iweke mfumo mzuri wa kushighilikia changamoto za kisheria zitakazoibuliwa wakati wa kampeni hiyo.

Katika kampeni hiyo, kata 80 na vijiji 240, vinatarajiwa kufikiwa na kampeni hiyo, iliyozinduliwa kitaifa tarehe 15 Februari mwaka huu. Kampeni hiyo inayotekelezaa chini ya Wizara ya Katiba na Sheria kwa kushirikiana na Shirika la Legal Services Facility (LSF) na mashirika mengine, imepewa jina la Samia, ili kuenzi mchango wa Rais Samia Suluhu Hassan, katika kutokomeza vitendo vya ukatili hasa kwa kina mama, watoto na makundi Maalum.

Ifahamike kuwa Kampeni hiyo inafanyika kwa miaka mitatu mfululizo, kuanzia Machi 2023 Hadi Desemba 2025.

 LSF kama mdau mkubwa wa upatikanaji wa haki imeshiriki Uzinduzi wa kampeni ya kitaifa ya Mama Samia Legal Aid. LSF inatoa ruzuku kwa mashirika ya wasaidizi wa kisheria 184 Tanzania Bara na Zanzibar na inawezesha watoa huduma za msaada wa kisheria zaidi ya 4500 kutoa huduma za msaada bure kwa wananchi. Pichani (watatu kulia waliosimama wakiwa wamevaa T-shirt) ni Mkurugenzi Mtendaji wa LSF, Lulu Ng'wanakilala katika picha ya pamoja na Waziri Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa Majaliwa wakati wa uzinduzi wa 'Mama Samia Legal Aid Campaign' uliofanyika 27.04.2023 Jijini Dodoma.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad