HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, April 28, 2023

JELA MAISHA KWA KUBAKA MTOTO WAKE WA KUFIKIA

 

Na Khadija Kalili
MAHAKAMA ya Wilaya ya Kibaha Mkoani Pwani imemuhukumu Dickson Chilongola (37) kabila Mkaguru ambaye ni fundi wa kuchomelea vyuma ambaye ni mkazi wa Zegereni Mlandizi Wilayani Kibaha Mkoani Pwani hukumu ya kwenda jela maisha , viboko 12 na kulipa fidia ya Mil.2, Hukumu hiyo imetolewa baada ya kupatikana na hatia ya kumbaka mtoto wake wa kufikia mwenye umri wa miaka 10 (jina limehifadhiwa)

Hukumu hiyo ya kesi ya jinai namba 13/2023 imetolewa leo Aprili 28, 2023 na Mheshimkwa Hakimu Judith Lyimo wa Mahakama ya Wilaya ya Kibaha Mkoani Pwani.

Hukumu hiyo imetolewa baada ya kusikiliza ushahidi wa pande zote, Mheshimiwa Hakimu Lyimo amesema kuwa amemtia hatiani mshitakiwa huyo kwa mujibu wa kifungu 130 (1), (2) (e) na kifungu 131 (1) cha kanuni ya adhabu sura ya 16 iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2022.

Aidha katika hukumu hiyo imeelezwa kuwa mtuhumiwa ametenda kosa hilo mnamo tarehe 01/02/2023 majira ya usiku mtaa wa Zegereni, Wilaya ya Kipolisi Mlandizi kwa kuingia chumbani kwa mtoto huyo kisha kumfanyia kitendo hicho cha kikatili.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad