HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, March 21, 2023

TANZANIA MWENYEJI MKUTANO WA KAMATI YA KUCHAKATA DATA ZA HALI YA HEWA DUNIANI

Mkurugenzi wa Idara ya Miundombinu kutoka Shirika la Hali ya Hewa Duniani (WMO) Dkt. Anthony Rea akizungumza wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa Kamati hiyo, unaonza leo Machi 20 -24, 2023 jijini  Arusha Tanzania.

 TANZANIA imekuwa mwenyeji wa mkutano wa Kamati ya Kuchakata Data za Hali ya Hewa Duniani, lengo ikiwa ni kuhakikisha data za hali ya hewa zinatumika ipasavyo na taasisi za hali ya hewa katika nchi wanachama wa Shirika la Hali ya Hewa Duniani (WMO) na kwa manufaa ya sekta mbalimbali. Mkutano huo unaojumuisha wajumbe kutoka nchi kumi na mbili (12).


Akizungumzia umuhimu wa mkutano huo kwa nchi, Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo na Mkurugenzi wa Huduma za Utabiri kutoka Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), Dkt. Hamza Kabelwa, amesema “kwanza ni kutangaza utalii wa nchi yetu ambapo wageni hawa watakuwa mabalozi wa vivutio vya Tanzania katika nchi zao, aidha, kutokana na changamoto kubwa za mabadiliko ya hali ya hewa na tabianchi, upatikanaji data sahihi za hali ya hewa ni muhmu kwa nchi zinazoendelea kama Tanzania katika kusaidia kukabiliana na mabadiliko hayo ili kutoa taarifa sahihi za hali ya hewa kwa maendeleo endelevu”.

Naye, Mwenyekiti wa Kamati hiyo Dkt. David Richardson, amesema Kamati anayoisimamia itajikita katika kusaidia kujenga uwezo na kusambaza taarifa za hali ya hewa kwa watumiaji wote ili kulinda maisha ya watu na mali zao.

Kwa upande wake, Dkt. Anthony Rea, Mkurugenzi wa Idara ya Miundombinu WMO amesema, majukumu ya kamati hiyo yanaenda sambamba na jitihada mbalimbali zinazoendelea kutekelezwa na WMO za kusaidia nchi katika kufanikisha upatikanaji wa data za uangazi za hali ya hewa ambazo zinazaa taarifa za hali ya hewa kwa matumizi ya nchi wanachama wa WMO.

Nchi zinazoshiriki mkutano huo unaofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Arusha (AICC) ulioanza leo Machi 20 hadi Machi 24, 2023 ni Australia, Brazil, Canada
Mwenyekiti wa Kamati ya kuchakata data za hali ya hewa duniani Dkt.David Richardson (Uingereza) akizungumza wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa Kamati hiyo, unaofanyika Arusha, Tanzania, Machi 20-24, 2023.
Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya kuchakata data za hali ya hewa duniani Dkt. Hamza Kabelwa (Tanzania) akizungumza wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa Kamati unaofanyika Arusha, Tanzania, leo Machi 20-24, 2023.
Wajumbe wa Kamati ya kuchakata data za hali ya hewa duniani wakifuatilia ufunguzi wa Mkutano wa Kamati hiyo, unaofanyika Arusha, Tanzania, leo Machi 20-24, 2023.
Picha ya Pamoja.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad