HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, March 21, 2023

NCHI 17 ZA KANDA YA AFRIKA WAJADILI MATUMIZI YA NISHATI SAFI KWENYE MAGARI

 

Picha ya pamoja.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Amos Makalla akizungumza wakati wa kufunguzi kikao kazi cha washiriki kutoka nchi 17 wakijadili masuala mbalimbali ya matumizi nishati safi katika magari. Kikao kazi hicho kimefunguliwa leo Machi 21, 2023 jijini Dar es Salaam.
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka (DART), Dkt. Edwin Mhede, akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo mara baada ya kufunguliwa kwa kikao kazi cha wawakilishi kutoka nchi 17 za kanda ya Afrika wa kujadili masuala ya matumizi ya Nishati safi na salama kwenye Magari. 
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Amos Makalla akizungumza wakati wa kufunguzi kikao kazi cha washiriki kutoka nchi 17 wakijadili masuala mbalimbali ya matumizi nishati safi katika magari. Kikao kazi hicho kimefunguliwa leo Machi 21, 2023 jijini Dar es Salaam.
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka (DART), Dkt. Edwin Mhede, akizungumza wakati wa ufunguzi wa kikao kazi cha washiriki kutoka nchi 17 wakijadili masuala mbalimbali ya matumizi nishati safi katika magari. Kikao kazi hicho kimefunguliwa leo Machi 21, 2023 jijini Dar es Salaam.

Mwakilishi wa Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi Rwanda, Janvier Twagirimana akizungumza wakati wa mkutano wa kujadili masuala ya matumizi ya Nishati safi na salama kwenye Magari. Pia ameelezea namna usafiri nchini Rwanda unavyofanya kazi ikiwa ni pamoja kutumia  Baiskeli zinazotumia umeme.
Baadhi ya washiriki wa mkutano wa kujadili masuala ya matumizi ya Nishati safi na salama kwenye Magari mkutano huo umefanyika jijini Dar es Salaam leo Machi 21, 2023.

WADU wa Usafiri kutoka nchi 17 za Kikanda Afrika wajadili masuala ya matumizi ya Nishati safi na salama kwenye Magari hapa nchini jijini Dar es Salaam leo Machi 21, 2023.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Amos Makalla akimwakilisha Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Angela Kairuki akizungumza wakati wa kufungua kikao kazi hicho amesema kikao kazi hicho kitajadili masuala ya matumizi ya umeme kwenye magari pamoja na matumizi ya betri ili kuepukana na uchafunzi wa mazingira na hali ya hewa.

Amesema magari yanayotumia umeme yatasaidia katika utunzaji wa mazingira na kuzuia uharibifu wa hali ya hewa ili kuendana na sera ya dunia inavyopambana na kukabiliana na uchafuzi wa mazingira.

Kwa upande wa Afya amesema kuwa Usafiri huo utaoanzia jijini Dar es Salaam utapunguza jamii kupata matatizo ya afya yanayotokana na uchafunzi wa hali ya hewa pamoja na kupunguza gharama za matibabu ya maradhi mbalimbali hasa yanayosababishwa na uchafuzi wa hali ya hewa.

Kwa Upande wa teknolojia ameeleza kuwa jamii inatakiwa kuwa na uelewa thabiti katika matumizi ya magari ya umeme ambapo kutatakiwa kuwe na muendelezo wa miundombinu pamoja na kuachana teknolojia ya kutumia mafuta ya magari. 

"Hii ni mhimu kwa ukuaji wa uchumi wa Tanzania pamoja na kupunguza gharama kwa utumiaji magari ya Umeme."

Magari ya usafiri wa umma yanawajibika na unachangia asilimia 67.4 ya uchagunzi mazingira unaotokana na hewa ukaa.

Akizungumzia kuhusiana na mradi wa Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka (DART) Makalla  amesema kuwa kunafaida kubwa za kujenga miundombinu jijini Dar es Salaam kwa sababu inasaidia wananchi kupata usafiri wa uhakika na kubeba watu wengi kwa wakati mmoja.

Amesema kuwa sekta ya usafiri inachangia kuleta uharibifu wa mazingira unaotokana na hewa ya Kabonidayoksaidi. 

Kwa upande wa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka (DART), Dkt. Edwin Mhede amesema kuwa katika Mjadala watajadili namna nchi za Afrika zinaweza kuja na matumizi ya magari yanayotumia nishati rafiki ili kupunguza kiwango cha hewa ya ukaa ambayo huzalishwa kila uchwao kutoka kwenye magari yanayotumia nishati ya mafuta.

Amesema mkutano huo unalenga kujadili kubadili matumizi ya mabasi au magari yanayotumia nishati ya umeme katika majiji yanayoendelea katika nchi za kikanda za Afrika.

Amesema nishati ya umeme inatoa kiwango cha kabonidayoksaidi kwa kiwango cha sifuri kwasababu  kunakuwa hakuna makelele wala uchafunzi wa hali ya hewa.

Akizungumzia kuhusiana na Changamoto zilizopo amesema kuwa uelewa wa jamii ni mdogo na Kila jambo linaeleweka kwa kujifunza na kupeana elimu, pia amesema kuanachangamoto za kimuundo ambapo changamoto hizo zinahitaji sera za uhakika, kama sera za kisheria, za kikodi na sera za uwekezaji, sera za fedha.

"Mazingira hayo lazima yafungamanishwe yote ili kutoa motisha ya wawekezaji ambao wanaweza kuwekeza kwenye sekta ya uzalishaji wa magari au watakao agiza magari kutoka nje ya nchi kule nchini kwaajili ya kutoa huduma.

Hata kwa Sisi waendeshaji tunahitaji kupata mazingira wezeshi ya kisera, ambayo yatapelekea kuona thamani ya fedha iliyowekezwa." Amesema Dkt. Mhede

Akizungumzia mradi wa BRT Dkt. Mhede amesema kuwa mtaji mkubwa uliopo Dar es Salaam ni miundombinu kukua kwa kasi na 'icon' Nembo ya BRT Afrika amesema ipo Dar es Salaam pia kwasiku moja wanahudumia watu zaidi ya laki mbili.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad