RC RUVUMA ASIKITISHWA UJENZI WA KITUO CHA AFYA KINGERIKITI KUWA CHINI YA KIWANGO, AAGIZA KUREKEBISHWA KASORO ZOTE ZILIZOJITOKEZA - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Saturday, March 4, 2023

RC RUVUMA ASIKITISHWA UJENZI WA KITUO CHA AFYA KINGERIKITI KUWA CHINI YA KIWANGO, AAGIZA KUREKEBISHWA KASORO ZOTE ZILIZOJITOKEZA

 

Jengo pacha la wodi ya mama na mtoto na upasuaji linaloendelea kujengwa katika kituo cha Afya Kingerikiti wilayani Nyasa ambalo Mkuu wa mkoa wa Ruvuma Kanal Laban Thomas hajaridhishwa na ubora wake.

Na Muhidin Amri,Nyasa
HALMASHAURI ya wilaya Nyasa,imekamilisha ujenzi wa nyumba moja ya kuishi familia tatu za watumishi wa idara ya afya katika kituo cha afya Kingerikiti kwa gharama ya shilingi milioni 94,605,427.41.


Hayo yamesemwa na Afisa mtendaji wa kata ya Kingerikiti Juma Ndimbo,wakati akitoa taarifa ya ujenzi wa nyumba hiyo kwa mkuu wa mkoa wa Ruvuma Laban Thomas.


Ndimbo alisema,ujenzi wa nyumba hiyo ulianza tangu mwezi machi 2022 kwa kutumia mfumo wa force account na imekamilika kwa zaidi ya asilimia 98 ambapo kwa sasa kazi iliyobaki ni kufunga taa 18 ambao umekwama kutokana na fedha zilizotengwa kwisha.


Alisema,kati ya fedha hizo shilingi milioni 46,683,075.41 zimetumika kununua vifaa vya viwandani,milioni 11,782,000,000 malipo ya fundi,milioni 34,810,200.00 vifaa visivyo vya viwandani na shilingi milioni 1,385,152.00 zimetumika kusafirisha vifaa.


Alisema katika utekelezaji wa ujenzi huo, wananchi wameshiriki kuponda kokoto na kupaki tripu 4 zenye thamani ya shilingi laki 9,kukusanya na kupakia mawe tripu 12 zenye thamani ya shilingi laki 6,kujaza kifusi kwa gharama ya shilingi laki 4,milundo(mbao)100 yenye thamani ya shilingi laki 2.


Aidha alieleza kuwa,wamepokea kiasi cha shilingi milioni 300 kwa ajili ya kujenga wodi ya Mama na mtoto na jengo la upasuaji ambapo majengo hayo yote yapo kwenye hatua ya ukamilishaji.

Alisema,mpaka sasa fedha zilizotumika ni shilingi milioni 270 ikiwa manunuzi ya vifaa vya viwandani vyenye thamani ya shilingi milioni 152,malipo ya vifaa visivyo vya viwandani shilingi milioni 84,kulipa mafundi shilingi milioni 24,stationaries shilingi laki 2 na usafirishaji shilingi milioni 8.


Ndimbo alisema,katika ujenzi wa mradi huo wananchi wameshiriki kuchimbua na kupakia mawe,kuponda na kupakia kokoto, kusogeza tofali,kuleta mbao 200 kusafisha eneo la ujenzi na kujaza kifusi.


Ndimbo alimweleza mkuu wa mkoa kuwa,kukamilika kwa miradi hiyo miwili kutaboresha utoaji wa huduma za afya kwa wakazi wa kata ya Kingerikiti na maeneo jirani na kupunguza adha ya makazi kwa watumishi wa umma watakaopelekwa kufanya kazi za kutoa huduma katika kituo hicho.

Kwa upande wake Mkuu wa mkoa wa Ruvuma Laban Thomos, amesikitishwa majengo hayo kujengwa chini ya kiwango na kuwataka watendaji waliosimamia ujenzi wa mradi huo kujitafakari kuhusiana na nafasi zao.


“mimi niseme tu kwa kweli sikifurahishwa hata kidogo na ujenzi wa mradi huu,yaani hapasehemu iliyojengwa vizuri ni kusimamisha kuta tu,lakini maeneo mengine ni ovyo kabisa”alisema Laban Thomas.

Kanal Laban,amemuagiza Mkuu wa wilaya ya Nyasa Filberto Sanga,kuhakikisha anasimamia ung’oaji wa milango yote mibovu na marekebisho katika kituo cha Kingerikiti na Hospitali ya wilaya Nyasa kabla kazi ya ujenzi wa miradi hiyo kuendelea.


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad