HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, March 14, 2023

DKT. NCHEMBA AKUTANA NA UJUMBE WA MOODY'S


Na Benny Mwaipaja, WFM, Dodoma

Taasisi ya kimataifa inayojihusisha na kuzifanyia tathimini nchi mbalimbali ili kujua uwezo wake wa kukopesheka katika masoko ya fedha ya Kimataifa, Moody’s, imetua nchini kwa ajili ya kufanya tathimini hiyo Tanzania.

Akizungumza wakati akiikaribisha timu ya wataalam kutoka Taasisi hiyo Jijini Dodoma, Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) amesema kuwa tathimini hiyo ni fursa kwa Tanzania kuweza kuyafikia Masoko ya fedha ya Kimataifa yatakayoiwezesha nchi kupata rasilimali fedha kwa ajili ya kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo ya wananchi.

Amesema kuwa uchumi wa Tanzania unaendelea kuimarika licha ya changamoto za Uviko 19 na Vita vya Ukraine na Urusi lakini pia Taifa limepiga hatua kubwa za kiuchumi, kidiplomasia, haki za binadamu na kisiasa.

Dkt. Mchemba alisema kuwa tathimini huru inayofanywa na Taasisi hiyo maarufu Duniani ya Moody’s inaiwezesha Tanzania kuaminiwa na Taasisi za fedha za kimataifa hivyo kuchochea uwekezaji ambao utakuza uchumi wa nchi pamoja na ajira kwa vijana.

Alisema kuwa ujio wa wataalam hao unajibu kiu ya Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, aliyeagiza nchi ifanyiwe tathimini ili kubaini uwezo wake wa kuyafikia masoko ya fedha ya kimataifa katika kuharakisha maendeleo ya watu.

Moody’s inaifanyia tathmini Tanzania kwa njia shirikishi itakayowezesha kutoa taswira halisi ya nchi na hatua ambazo imepiga kiuchumi, kijamii na kisiasa.

Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), (kulia), akisalimiana na Kiongozi wa jopo la wataalam waliowasili nchini kufanya tathimini ya uwezo wa Tanzania kukopesheka kwenye masoko ya Kimataifa (credit rating) ya Moody’s, Bw. John Walsh, Jijini Dodoma.

Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), akizindua zoezi la Taasisi ya kufanya tathimiji ya uwezo wa nchi kukopesheka kwenye masoko ya Kimataifa (credit rating) ya Moody’s, Jijini Dodoma. Kulia ni Kiongozi wa Timu hiyo Bw. John Walsh. Moody’s wapo nchini kuifanyia Tanzania Credit Rating.

Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), akizungumza na wataalam wa kufanya tathimini ya uwezo wa nchi kukopesheka kwenye masoko ya Kimataifa (credit rating) ya Moody’s, Bw. John Walsh (kulia) na Bw. Aurelien Mali, Jijini Dodoma. Moody’s wameanza kazi leo ya kuifanyia Tanzania Credit Rating.

Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), akisalimiana na Mtaalam wa kufanya tathimini ya uwezo wa nchi kukopesheka kwenye masoko ya Kimataifa (credit rating) ya Moody’s Bw. Aurelien Mali, Jijini Dodoma. Katikati ni Kiongozi wa Timu hiyo Bw. John Walsh. Moody’s wapo nchini kuifanyia Tanzania Credit Rating.

Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na timu ya wataalam kutoka Taasisi ya Kimataifa ya Kufanya Tathimini ya Uwezo wa Tanzania kukopesheka kwenye masoko ya Kimataifa (credit rating) Bw. John Walsh (wa tatu kushoto) akifuatiwa na Bw. Aurelien Mali na Kamishna Idara ya Usimamizi wa Deni la Taifa, Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Japhet Justin. Kulia ni Naibu Gavana wa Benki kuu ya Tanzania Dkt. Yamungu Kayandabila, Naibu Gavana wa Benki kuu ya Tanzania, Bi. Sauda Msemo na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Lawrence Mafuru, baada ya kukutana Jijini Dodoma kwa ajili ya kuanza kazi ya tathimini hiyo.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad