HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, March 14, 2023

DCB Elimu Mpango Mzima na Mama Samia yazidi kuchanja mbuga
Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Songoro Mnyonge ( wa pili kushoto) akikabidhi cheti cha shukrani kwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya Biashara ya DCB, Zawadia Nanyaro ( katikati ) na Mkurugenzi Mtendaji wa benki hiyo, Isidori Msaki kilichotolewa na Uongozi wa Shule ya Mtakuja kwa kutambua mchango wa DCB kwa maendeleo ya shule hiyo. Ilikuwa ni baada ya kupokea msaada wa madawati 30 shuleni hapo, Kunduchi, Dar es Salaam leo. Wengine kutoka kushoto ni .Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni, Hanifa Suleimani Hamza na Kaimu Ofisa Elimu wa Manispaa hiyo, Msingwa Ibrahimu.

Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mawasiliano wa Benki ya Biashara ya DCB, Rahma Ngassa akizungumza na wanafunzi wa shule ya msingi Mtakuja baada ya kuwakabidhi msaada wa madawati 30 ikiwa ni muendelezo wa kampeni yake inayoendelea ya elimu iitwayo “Elimu Mpango Mzima na Mama Samia” jijini leo.
Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mawasiliano wa Benki ya Biashara ya DCB, Rahma Ngassa pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa wakijitambulisha ambapo wakipata nafasi ya kuelezea huduma mbalimbali za kibenki zinazotolewa na benki hiyo.
Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Songoro Mnyonge akizungumza kabla ya kupokea msaada wa madawati 30 kwa ajili ya shule ya msingi Mtakuja yaliyotolewa na Benki ya Biashara ya DCB.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya Biashara ya DCB, Zawadia Nanyaro akizungumza katika hafla hiyo.
.Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Songoro Mnyonge ( wa pili kushoto) akikata utepe kuashiria makabidhiano ya msaada wa Madawati 30 kutoka Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya Biashara ya DCB, Zawadia Nanyaro ( katikati) kwa ajili ya Shule ya Msingi Mtakuja shuleni hapo, Kunduchi, Dar es Salaam leo. Wanaoshangilia kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni, Hanifa Suleimani Hamza, Mkurugenzi Mtendaji wa benki hiyo, Isidori Msaki, Kaimu Ofisa Elimu wa Manispaa hiyo, Msingwa Ibrahimu na Mkuu wa Shule ya Msingi Mtakuja, Anna Nyomeye.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya Biashara ya DCB, Zawadia Nanyaro, akishikana mikono na wanafunzi wa Shule ya msingi Mtakuja muda mfupi baada ya kukabidhi msaada wa madawati 30 ikiwa ni muendelezo wa kampeni yake inayoendelea ya elimu iitwayo “Elimu Mpango Mzima na Mama Samia” shuleni hapo Leo.
Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Songoro Mnyonge (kushoto), akizungumza na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Benki ya Biashara ya DCB, Zawadia Nanyaro huku Mkurugenzi Mtendaji wa benki hiyo, Isidori Msaki (wa tatu kushoto akiangalia), katika hafla ya makabidhiano ya msaada wa madawati 30 kwa ajili ya Shule ya Msingi Mtakuja ikiwa ni mwendelezo wa kampeni yake inayoendelea ya ‘ Elimu Mpango Mzima na Mama Samia ’ shuleni hapo, Kunduchi, Dar es Salaam leo.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad