HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Sunday, December 11, 2022

MIAKA 61 YA UHURU NA ONGEZEKO LA WATANZANIA MILIONI 61

 


Na John Walter-Manyara.
Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa TAKUKURU mkoa wa Manyara hii leo imefanya zoezi la upandaji miti kwenye mazingira ya ofisi zao na shule mbalimbali wilayani Babati kwa lengo la kuadhimisha siku ya maadili na haki za binadamu inayokwenda na kauli mbiu isemayo ‘’kuzuia rushwa ni jukumu lako na langu tutimize wajibu wetu.’’

Zoezi hilo la upandaji miti limeongozwa na Kaimu Kamanda wa TAKUKURU mkoa wa Manyara Moses Oguda, ambapo amesema upandaji wa miti unasaidia kuboresha mazingira lakini pia kuweka alama ya ushirikiano mzuri na jamii katika harakati za kupambana na kuzuia rushwa.

Aidha mkuu wa dawati la elimu kwa umma TAKUKURU mkoani hapa Richard Samila, amesema kwa sasa wakazi wa mkoa wa Manyara wanauelewa mkubwa juu ya elimu ya rushwa na kwamba wametengeneza mazingira mazuri ili mwananchi yeyote anayepata changamoto aweze kuwafikia kwa urahisi.

Aidha Samila amesisitiza utunzaji wa mazingira kwani uharibifu wa mazingira ni kichocheo kikubwa cha vitendo vya rushwa katika jamii.

Nao baadhi ya walimu wa shule za Msingi Kwang’ na Harambee waliohudhuria katika hafla hiyo ya upandaji wa miti wameoneshwa kufurahishwa na zoezi hilo wakieleza litasaidia kuboresha mazingira kwenye maeneo ya shule na kuwashukuru viongozi wa takukuru kwa kutambua umuhimu wao kwenye harakati za kupambana na kutokomeza rushwa.

Siku ya maadili na haki za binadamu huadhimishwa kila Desemba 10 ya kila mwaka ikiwa na lengo la kutambua na kusisitiza utekelezwa wa haki za binadamu katika jamii na kukemea vitendo vyote vinavyoashiria uvunjifu wa haki za binadamu, ikiwemo vitendo vya kutoa na kupokea rushwa ambavyo vinapingwa vikali na taasisi ya TAKUKURU.

Maadhimisho ya siku ya haki za binadamu yalianzishwa mnamo mwaka 1948 miaka michache baada ya kumalizika kwa vita vya pili vya dunia ikiwa na lengo la kuhakikisha ulimwengu hauingii tena kwenye migogoro na kufanya dunia kuwa sehemu salama na sheria mbalimbali zilitungwa ili kutetea haki za binadmu ulimwenguni.

Kwasa ni takribani miaka 74 tangu maadhimisho ya siku hii yaanze lakini bado ulimwengu unakabiliwa na machafuko kwenye maeneo mbalimbali machafuko ambayo chanzo chake kikuu ni rushwa, ulafi wa madaraka, vitendo vinavyochochea ukiukwanji wa haki za binadamu kama vile kupata elimu,mazingira bora ya kuishi na fursa za ajira.

 No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad