HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, November 28, 2022

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA MGENI RASMI KONGAMANO LA UWEKEZAJI

 

Mkuu wa Kitengo cha Ukuaji wa Uchumi Jumuishi UNDP, Emmanuel Nnko, akizungumza na  waandishi wa habari juu ya kongamano la la uwekezaji linalotarajiwa kufanyika Novemba 30, 2022 Jijini Dar es Salaam kulia kwake ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) John Mnali

WAZIRI Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa anatarajiwa kwa mgeni rasmi katika Kongamano maalum la kuhamasisha na kukuza Uwekezaji na biashara kwa sekta kipaumbele zenye mlengo wa maendeleo endelevu Tanzania.

Kongamano hiyo lililoandaliwa na Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) kwa kushirikiana na Shirika la Umoja wa Taifa linaloshughulikia maendeleo la UNDP na Wizara ya Uwekezaji Viwanda na Biashara, linatarajiwa kufanyika Novemba 30, 2022 katika Ukumbi wa Mikutano wa Hoteli ya Rotana jijini Dar es Salaam.

Baada ya kongamano hilo pia kutakuwa na zoezi la kutembelea miradi Desemba Mosi 2022.

Lengo la mkutano huo ni kutangaza fursa za biashara na uwekezaji zenye mlengo ya maendeleo endelevu zilizopo hapa nchini kwa wafanyabiashara na wawekezaji wa kutoka nchi mbalimbali duniani.

Pia kutangaza fursa ambazo zipo katika sekta za kipaumbele zenye mlengo wa maendeleo endelevu ikiwa ni pamoja na sekta ya Kilimo na chakula, Miundombinu, Nishati, Elimu na huduma.

Kongamano hilo halina kiingilio lakini tungependa wale wote ambao wangependa kuhudhuria kutuma uthibitisho. Tunaomba wote waliothibitisha kuhudhuria kufika bila kukosa fursa hii muhimu kwa nchi na wawekezaji wetu.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad