Mkurugenzi Mkuu wa kampuni ya GF
Trucks & Equipments Ltd, Imran Karmal ,amepata tuzo ya kuwa
Mtendaji Mkuu Bora namba 2 wa mwaka 2022 wakati wa Tuzo zilizofanyika
jijini Dar es salaam.
Tuzo hizo zilizoandaliwa na taasisi ya
kimataifa ya KPMG kwa kwa kushirikiana na Tasisi ya Mameneja nchini
Tanzania (Institute of Manager Tanzania )
Ushindi huo wa Karmal ni
zawadi kwa wafanyakazi wote wa kampuni anayoiongoza ya GF Trucks &
Equipment Ltd na furaha kwake kwani bila wafanyakazi imara hakuna
kiongozi imara alimaliza Karmal.
Hii ni mara ya pili kwani mwaka
jana alishika nafasi ya 9 kati ya CEO 100 waliokuwa wakiwania nafasi
hiyo na tunashukuru mungu mwaka huu kuwa namba mbili wakati nafasi ya
kwanza ikishikwa na Mkurugenzi wa benki ya CRDB,Abdulmajid Nsekela
Baadhi ya wafanyakazi walifurah Boss wao kuibuka kidedea kwani wanaamini mwakani katika Tuzo zinazofata ataibuka namba 1.
Karmali anaiongoza kampuni ya GF inayomiliki Kiwanda cha kuunganisha magari
kilichopo Kibaha mkoani Pwani na pia ni wauzaji wa magari ya FAW,HONG
YAN ambayo kwa sasa yanatengenezawa katika kiwanda kilichopo Kibaha
mkoani Pwani pamoja na mitambo ya XCMG Waziri
wa Biashara na Maendeleo ya Viwanda Zanzibar ,Omar Said
Shaban(katikati) akimkabidhi Mkurugenzi wa kampuni ya GF Trucks &
Equipment’s Ltd ,Imran Karmal tuzo ya CEO bora namba 2 wa mwaka 2022
wakati wa hafla ya tuzo za Tanzanite Top 100 CEO zilizofanyika jijini
Dar es salaam.Kushoto ni mwenyekiti wa Tanzania Institute of
Manager(TIM) Deogratius Kilawe.Picha na Said Khamis
Mkurugenzi wa kampuni ya GF Trucks & Equipment’s Ltd, Imran Karmal akizungumza wakati wa hafla kupokea tuzo hizo
3-Mkurugenzi wa GF akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa kampuni hiyo.
Monday, November 28, 2022

MKURUGEZI GF TRUCKS & EQUIPMENTS,IMRAN KARMAL ASHINDA TUZO YA CEO 2022
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment