HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, November 23, 2022

UPIMAJI NA MATIBABU YA MAGONJWA YA MOYO KATIKA MIKOA YA MTWARA NA LINDI

 

Wataalamu wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa kushirikiana na wenzao wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda Mtwara pamoja na Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Lindi – Sokoine watafanya upimaji na matibabu ya moyo kwa watoto na watu wazima.

Mkoani Mtwara upimaji utafanyika kuanzia tarehe 28 hadi 30 Novemba, 2022 kuanzia saa mbili kamili asubuhi hadi saa 10 kamili jioni katika viwanja vya Hospitali ya Rufaa ya Kanda Mtwara. Kwa taarifa zaidi kuhusu upimaji utakaofanyika mkoani Mtwara wasiliana kwa namba 0685921947 Dkt. Maximilliana Mwenda na 0686732326 Bi. Eshe Mnyanga.

Tarehe 2 hadi 4 Desemba, 2022 upimaji na matibabu ya moyo utafanyika mkoani Lindi katika viwanja vya Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Lindi – Sokoine kuanzia saa mbili kamili asubuhi hadi saa 10 kamili jioni. Kwa taarifa zaidi kuhusu upimaji utakaofanyika mkoani Lindi wasiliana kwa namba 0786066182 Dkt.Godwin Macheku na 0653134711 Dkt. Martin Kazi.

Tutakuwa na wataalamu wa lishe ambao watatoa elimu ya lishe bora ambayo itawapa wananchi uelewa na kufuata mtindo bora wa maisha utakaowasaidia kuepukana na magonjwa ya moyo ambayo ni moja ya magonjwa yasiyoambukiza na mtu anaweza kuyaepuka kwa kufuata ushauri wa kitaalamu.

Watakaogundulika kuwa na matatizo ya moyo watafanyiwa uchunguzi zaidi na kupatiwa matibabu hapohapo au kupewa rufaa ya kuja kutibiwa katika Taasisi yetu.

Tunawaomba wananchi mjitokeze kwa wingi kupima afya zenu kujua kama mna matatizo ya moyo ili kuanza matibabu mapema kwa atakayebainika kuwa mgonjwa.


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad