Na Mwandishi Maalum, Morogoro
TUME
ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imewataka wasimamizi wa uchaguzi na
wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi kutoka katika Kata zinazotaraji
kufanya uchaguzi mdogo wa udiwani Desemba 17, 2022 kutofanya kazi ya
uchaguzi kwa mazoea, badala yake wazingatie sheria, kanuni za uchaguzi
pamoja na maelekezo ya Tume katika utendaji wao.
Tume
pia imewataka wasimamizi wa nchaguzi na wasimamizi wasaidizi wa
uchaguzi kuhakikisha wanavishirikisha Vyama vyote vya Siasa na wadau
wengine wa uchaguzi ili kurahisha utekelezaji wa majukumu yao.
Hayo
yamesemwa na Mjumbe wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Adv. Magdalena
Rwebangira wakati akifungua mafunzo ya siku tatu ya wasimamizi wa
Uchaguzi na wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi ngazi ya Kata yanayofanyika
Mkoani Morogoro.
Adv.
Rwebangira amesema Uchaguzi ni mchakato unaojumuisha, hatua na taratibu
mbalimbali za kufuatwa na kuzingatiwa kwani hatua na taratibu hizo
ndiyo msingi wa uchaguzi kuwa mzuri, wenye ufanisi na hivyo kupunguza
kama siyo kuondoa kabisa malalamiko au vurugu wakati wote wa mchakato wa
uchaguzi.
“Nachukua
nafasi hii kuwaasa kuwa pamoja na uzoefu ambao baadhi yenu mnao katika
uendeshaji wa uchaguzi, ni vyema mhakikishe mnazingatia maelekezo
mtakayopewa na Tume badala ya kufanya kazi kwa mazoea”,alisema Adv.
Rwebangira.
Aidha
amewataka kujiamini na kufanya kazi kwa weledi, na kwamba katika
utendaji wa majukumu yao wanapaswa kuzingatia Katiba ya Nchi, Sheria za
Uchaguzi na Kanuni zake, Maadili ya Uchaguzi na Maelekezo mbalimbali
yanayotolewa na Tume na kuongeza kua jambo hilo lisiishie katika mafunzo
na nadharia bali ionekane kufuatiwa katika kutenda.
“Sanjari
na hilo nawaasa kukumbuka kuvishirikisha Vyama vya Siasa na wadau
wengine wa uchaguzi katika maeneo yenu katika masuala ya kiuchaguzi
ambayo wanastahili kushirikishwa kwani jambo hilo litawarahisishia sana
utekelezaji wa majukumu yenu,”alisema Adv Rwebangira.
Wasimamizi
hao wametakiwa kuhakikisha wanayatambua na kuyajua vizuri maeneo
ambayo chaguzi utaendeshwa ikiwemo hali ya miundombinu ya kufika katika
Kata na hasa Vituo vya kupigia kura.
“Mfanye
utambuzi wa vituo vya kupigia kura mapema ili kubaini mahitaji maalum
ya vituo husika kwa lengo la kuhakikisha mpangilio mzuri ambao
utaruhusu uchaguzi kufanyika kwa utulivu na amani,”alisema Adv.
Rwebangira.
Mjumbe
wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Adv. Magdalena Rwebangira pia amewataka
wasimamizi hao kuhakikisha kuwa wanaajiri watendaji wa vituo wenye
weledi, wanaojitambua na kwa kadri inavyowezekana kuacha undugu au
upendeleo kwa ndugu na jamaa ambao hawana sifa za kufanya shughuli za
uchaguzi.
Alisema
jambo muhimu wanalotakiwa kuzingatia Wasimamizi hao wa uchaguzi ni
kujiamini, kufanya kazi kwa weredi na kuzingatia Katiba ya nchi, sheria
za uchaguzi na kanuni zake, maadili ya uchaguzi pamoja na maelekezo
mbalimbali yanayotolewa na Tume.
Aidha
Mjumbe wa Tume hiyo ya uchaguzi, aliwasisitizia wasimamizi hao wa
uchaguzi kuhakikisha wanafanya utambuzi wa vituo vya uchaguzi mapema kwa
lengo la kuhakikisha mpangilio mzuri ambao utaruhusu uchaguzi kufanyika
kwa utulivu na amani.
Naye
Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Usimamizi wa Uchaguzi kutoka Tume ya
Taifa ya Uchaguzi, Bw. Stephen Elisante, akizungumza kwa niaba ya
Mkurugenzi wa Uchaguzi alisema uchaguzi huo mdogo wa udiwani utafanyika
katika Kata 12 za Tanzania Bara ila waliopo katika mafunzo hayo Mkoani
Morogoro ni kutoka katika Kata sita za Vibaoni – Halmashauri ya Mji wa
Handeni, Lukozi – Halmashauri ya Wilaya ya Lushoto, Misugusugu –
Halmashauri ya Mji wa Kibaha, Majohe - Halmashauri ya Jiji la Dar es
Salaam, Mnyanjani - Halmashauri ya Jiji la Tanga na Dunda - Halmashauri
ya Wilaya ya Bagamoyo.
Mapema
kabla ya ufunguzi wa Mafunzo hayo watendaji w uchaguzi hao walikula
kiapo cha kutunza siri na kiapo cha kujitoa uanachama wa vyama vyao vya
siasa mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi Mkoa wa Morogoro, Mhe. Japhet Bwire
Manyama.
Mjumbe
wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Adv. Magdalena Rwebangira akizungumza
wakati wa kufungua mafunzo ya siku tatu ya wasimamizi Uchaguzi na
wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi pamoja na watendaji wengine wa Uchaguzi
ngazi ya Jimbo na Kata ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya uchaguzi mdogo
wa udiwani unaotaraji kufanyika tarehe 17 Desemba, 2022. Mafunzo hayo
yanayohusisha washiriki 42 kutoka Halmashauri sita za Jiji la Dar es
Salaam, Bagamoyo mji, Kibaha Mji, Handeni Mji, Jiji la Tanga na Lushoto
yanafanyika Mkoani Morogoro.
Mjumbe
wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Adv. Magdalena Rwebangira akizungumza
wakati wa kufungua mafunzo ya siku tatu ya wasimamizi Uchaguzi na
wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi pamoja na watendaji wengine wa Uchaguzi ngazi
ya Jimbo na Kata ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya uchaguzi mdogo wa
udiwani unaotaraji kufanyika tarehe 17 Desemba, 2022. Mafunzo hayo
yanayohusisha washiriki 42 kutoka Halmashauri sita za Jiji la Dar es
Salaam, Bagamoyo mji, Kibaha Mji, Handeni Mji, Jiji la Tanga na Lushoto
yanafanyika Mkoani Morogoro. Kushoto ni Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya
Usimamizi wa Uchaguzi, Stephen Elisante na wengine kulia ni Mwakilishi
wa Mkurugenzi wa Utawala na Usimamizi wa Rasilimali watu wa Tume,
Felister Ishuza na Mwenyekiti wa Mafunzo hayo ambaye pia ni Msimamizi wa
Uchaguzi Jimbo la Handeni, Maryam Ahmad Ukwaju.
Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Usimamizi wa Uchaguzi, Stephen Elisante akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo.
Mwenyekiti
wa Mafunzo hayo ambaye pia ni Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Handeni,
Maryam Ahmad Ukwaju akizungumza wakati wa mafunzo hayo.
Sehemu
ya washiriki ambao ni Wasimimizi wa uchaguzi na Wasimamizi wasaidi wa
Uchaguzi kutoka Halmashauri sita za Jiji la Dar es Salaam, Bagamoyo mji,
Kibaha Mji, Handeni Mji, Jiji la Tanga na Lushoto yanafanyika Mkoani
Morogoro wbakifuatilia mafunzo hayo.
Sehemu
ya washiriki ambao ni Wasimimizi wa uchaguzi na Wasimamizi wasaidi wa
Uchaguzi kutoka Halmashauri sita za Jiji la Dar es Salaam, Bagamoyo mji,
Kibaha Mji, Handeni Mji, Jiji la Tanga na Lushoto yanafanyika Mkoani
Morogoro wbakifuatilia mafunzo hayo.
Hakimu
Mkazi Mfawidhi wa Mkoa wa Morogoro, Japhet Bwire Manyama akiongoza
kiapo cha kujitoa uanachama wa vyama vya siasa na kutunza siri kwa
wazimamizi na wasimamizi wasaidi wa uchaguzi wakati wa mafunzo ya
wasimamizi hao kutoka Halmashauri sita za Jiji la Dar es Salaam,
Bagamoyo mji, Kibaha Mji, Handeni Mji, Tanga Jiji na Lushoto ambao
wanataraji kufanya uchaguzi mdogo katika kata zao Desemba 17,2022.
Wasimamizi
wa Uchaguzi na Wasimamizi wasaidizi wa Uchaguzi wakilakiapo cha kujitoa
uanachama wa vyama vya siasa na kutunza siri mbele ya Hakimu Mkazi
Mfawidhi wa Mkoa wa Morogoro, Japhet Bwire Manyama wakati
wa mafunzo ya wasimamizi hao kutoka Halmashauri sita za Jiji la Dar es
Salaam, Bagamoyo mji, Kibaha Mji, Handeni Mji, Tanga Jiji na Lushoto
ambao wanataraji kufanya uchaguzi mdogo katika kata zao Desemba 17,2022.
No comments:
Post a Comment