TACHA YAHITIMISHA MAFUNZO MAALUM YA UMILIKI NA MATUMIZI SILAHA - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, November 21, 2022

TACHA YAHITIMISHA MAFUNZO MAALUM YA UMILIKI NA MATUMIZI SILAHA


 Mwindaji pekee wa kike kutoka TACHA Bi. Fina Felix akipokea cheti cha kufuzu mafunzo ya umiliki na utumiaji wa silaha kutoka kwa ASP Hamis Luyeko (kushoto.)
ASP  Hamis Luyeko akizuungumza wakati wakufunga mafunzo hayo amewapongeza TACHA kwa kuonesha nidhamu kwa jeshi la polisi na kuwataka watanzania kujiunga na chama hicho.


 

CHAMA cha Uhifadhi na Uwindaji Tanzania (CHATA,) kimeiomba Serikali kutoa leseni za umiliki wa silaha kwa wanaopata mafunzo na kutunukiwa vyeti ili waweze kutumia silaha hizo kwa umahiri zaidi bila kudhuru wanyama na raia.

Hayo yameelezwa na Mwenyekiti wa Chama cha Uhifadhi na Uwindaji Tanzania (CHATA,) Kanali Thomas Ndonde (rtd) mara baada ya kufungwa kwa mafunzo ya siku mbili ya kuwajengea uwezo, umahiri na kujiamini zaidi katika matumizi ya silaha yaliyofanyika katika viwanja vya Shabaha jijini Dar es Salaam na kueleza, chama hicho kimekuwa kikihakikisha wanachama wanapata mafunzo na wanaofanya vizuri wanapata vyeti vinavyotolewa na jeshi la polisi.

‘’TACHA inajumuisha wawindaji wenyeji wanaofanya shughuli za uwindaji kwa kufuata sheria na miongozo ya uwindaji kwa kuzingatia matakwa ya Serikali….Na mafunzo haya ni ya lazima kwa mujibu wa sheria tunalishukuru jeshi la polisi kwa kutoa mafunzo haya ya nadharia na vitendo kwa siku mbili na kutunuku vyeti na  tutakaguliwa kwa kipindi cha miaka mitano ili kujenga ufanisi zaidi .’’ Amesema.

Pia ameishauri Serikali kutoa leseni kwa raia waliopata mafunzo na kupata vyeti ili waweze kutumia silaha zao bila kudhuru wanyama na raia na kuwataka watanzania kujiunga na TACHA ili waweze kupata mafunzo hayo.

Awali mkufunzi wa mafunzo hayo ASP Hamis Luyeko alikipongeza chama hicho kwa kuonesha nidhamu kwa Jeshi la Polisi na kufanikisha mafunzo hayo na kuwataka raia kujiunga na TACHA ili waweze kupata mafunzo, leseni na vibali vingine vinavyohusu silaha.  

Kwa upande wake Mratibu msaidizi wa  Umahiri wa Utumiaji na Utunzaji wa Silaha za moto za Kiraia nchini kutoka Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Polisi Tanzania (TPFCS,) Ravent Vedasto ameipongeza TACHA kwa kuhakikisha kila mwanachama anapata mafunzo hayo ambayo ni kwa mujibu wa sheria ya The Firearms and Ammunition Control Act ya mwaka 2015.

‘’Ni lazima kwa wamiliki wa silaha kupata mafunzo haya na kupatiwa vyeti, hadi sasa raia wapatao 5000 wamepata mafunzo haya na kwa miezi mitatu kuanzia Julai mwaka huu hadi Oktoba raia 2000 wamepata mafunzo…mpango ni kuwafika nchi nzima kwa zoezi hili ifikapo 2025/2026.’’ Amesema.

Amewataka raia kujiunga na TACHA ili waweze kupata mafunzo hayo muhimu ya kuwajengea uwezo, umahiri na kujiamini zaidi na kupatiwa vyeti mara baada ya kuhitimu mafunzo hayo.

Mwindaji pekee wa kike kutoka TACHA ambaye amefuzu vyema katika mafunzo hayo kwa kupata alama za juu na kukabidhiwa cheti Bi. Fina Felix amesema, amejifunza uwindaji akiwa mdogo kutoka kwa familia yake na amekuwa mahiri katika uwindaji licha ya jamii kuona fani hiyo ni ya wanaume.

‘’Wanawake tunaweza kufanya kila kitu, nitoe wito kwa wanawake wengi zaidi kujifunza fani hii na kuifanya kazi hiyo kuwa sehemu ya kujiingizia kipato.’’ Amesema.

Kwa upande wake mwakilishi wa kampuni ya Orxy ambao wamedhamini mafunzo hayo Gracious Matunda amesema udhamini huo unakwenda sambamba na kampeni ya utunzaji na uhifadhi wa mazingira kwa wawindaji na wananchi kwa ujumla na wanahahimiza kutumia nishati ya gesi kwa kupikia kwa gharama nafuu na salama zaidi na kuacha kukata miti ili kutunza mazingira na kuepuka na mabadiliko ya tabia Nchi yanayoleta athari mbalimbali ikiwemo ukame.
mafunzo yakiendelea.
Mwakilishi wa kampuni ya Orxy ambao wamedhamini mafunzo hayo Gracious Matunda akizungumza mara baada ya kufungwa kwa mafunzo hayo na kueleza kuwa udhamini huo unakwenda sambamba na kampeni ya utunzaji na uhifadhi wa mazingira kwa wawindaji na wananchi kwa ujumla na wanahahimiza kutumia nishati ya gesi kwa kupikia kwa gharama nafuu na salama.
 

 

 

 

 

 

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad