HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, November 21, 2022

MANISPAA YA IRINGA YANG’ARA TUZO ZA USAFI KITAIFA, YASHIKA NAFASI YA PILI

 Mstahiki Meya wa Manispaa ya Iringa Mhe.Ibrahim Ngwada pichani akikabidhiwa cheti cha ushindi wa pili katika mashindano ya Taifa ya afya na usafi wa mazingira 2022, kundi la Halmashauri za Manispaa Tanzania bara.

Hii ndio tuzo waliyopewa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa
Viongozi mbalimbali kutoka Mkoa wa Iringa wakionyesha tuzo walizopata za usafi wa Mazingira na afya

N Fredy Mgunda,Iringa.
MANISPAA ya Iringa imepata zawadi ya cheti na fedha kiasi cha shilingi milioni kumi (10,000,000) Ikiongozwa na mshindi wa kwanza Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga ambao wamejipatia cheti na fedha shilingi milioni 15 na mshindi wa tatu ni Halmashauri ya Manispaa ya Moshi amboyo imepsta cheti na sh milioni tano.

Tukio hilo la ugawaji wa vyeti na zawadi lilifanywa na Mgeni rasmi Naibu katibu Mkuu wizara ya Afya Dkt.Seif Shekalaghe

Novemba 19,2022 Katika ukumbi wa Jakaya Kikwete Jijini Dodoma kwenye kilele cha wiki ya usafi kitaifa na maadhimisho ya siku ya choo Duniani.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad