HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, October 3, 2022

Watanzania jitokezeni kutalii mbuga za Saadan

Na Mwandishi Wetu
WATANZANIA wametakiwa kujitokeza kushiriki kwenda kwenye vivutio vya utalii lengo likiwa ni kumuunga mkono Rais Mama Samia Suluhu Hassan kupitia filam ya Royal Tour ambayo imeitangaza Tanzania.

Wito umetolewa Jijini Dar es Salaam na Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana Kata ya Mabwepande Jimbo la Kinondoni (UVCCM), Andrew Mashimba, wakati akizungumza na vyombo vya habari kuhusiana na mafanikio ya Serikali ya awamu ya Sita ikiwemo ukuzazaji wa sekta ya Utalii nchini.

Kiongozi huyo alisema lengo la kuandaa matembezi hayo ya kwenda Sadaan ni kwa lengo la kumuunga mkono mama Samia katika jitihada zake za kutangaza utalii wa Nchi yetu na kutengeneza desturi ya kutembelea vitu vyetu wenyewe.

Alisema ni vyema watanzania tukapenda vya kwetu kuliko kunyamaza kimya na kuishia kulalamika wakati vivutio vyetu vipo na ni bora.

Katibu wa UVCCM Mabwepande Ramadhani Kindamba alisema kuwa wamejipanga vizuri katika kuhakikisha jambo hili linatimia.

"Sisi tukiwa vijana lazima tumuunge mkono mama na kuhakikisha kila kitu kinaenda sawa hivyo uchaguzi umeisha na sasa kazi 'Iendelee'.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad