Kampuni ya simu za mkononi ya
Airtel leo imezindua maadhimisho ya Wiki ya Huduma kwa wateja ambapo kwa
wiki nzima hii, Airtel itakuwa ikifanya maonyesho ya huduma na bidhaa
zake.
Akizungumza leo jijini Dar es Salaam wakati wa uzinduzi wa
maadhimisho hayo, Mkurugenzi wa Kitengo cha Huduma kwa wateja Airtel
Tanzania Adriana Lyamba alisema kuwa hii Wiki ya Huduma kwa wateja
inatoa fursa nyingine kwa Airtel kujiweka karibu na wateja wake ambao ni
watu muhimu sana kwenye biashara yetu. ‘Huku kauli mbiu ya Wiki ya
Huduma kwa wateja ikiwa ni furahia huduma, Airtel inajivunia kwa
Watanzania kuwa wateja wetu na tunahidi kuendelea kutoa huduma bora na
za kisasa, alisema Lyamba.
‘Moja kati ya hatua ambazo Airtel
tuweza kuzipiga vizuri na tunazojivunia ni teknolojia. Tunayo furaha
kubwa kuwa kwa sasa wateja wetu wanaweza kutumia teknolojia na
kujihudumia papo hapo. Wateja wa Airtel kwa wanaweza kupata LUKU TOKEN
kwa kujihudumia mwenyewe, kurudisha muamala uliokosewa, kurudisha laini
ya simu iliyopotea bila kuongea na mtoa huduma wa Airtel. Huduma zote
hizi mteja anaweza kuzipata kwa urahisi na hii ni moja ya faraja yetu
tunayojivunia kwenye teknolojia kama watoa huduma, Lyamba alisema.
Meneja
Huduma kwa wateja Celina Njuju alisema kuwa kwenye maadhimisho haya ya
wiki ya huduma kwa Airtel itajikita kwenye kushiriki kwenye matukio
yanaogusa jamii moja moja. ‘Airtel kwa muda mrefu tumekuwa
tukishirikiana na jamii inayotuzunguka kwenya masuala ya afya na elimu.
Kwenye wiki hii ya maadhimisho ya wiki ya Huduma kwa wateja, tutaembelea
na kuwapa faraja watoto wanaoishi kwenye mazingira magumu kama ishara
ya kuonyesha upendo, Njuju alisema.
Njuju aliongeza kuwa ili
kuendana na kauli mbiu ya Wiki ya Huduma kwa wateja kwa mwaka huu ya –
Sherehekea Huduma, Airtel itaendelea kutoa huduma zenye ubora wa ili
kuendelea kuendana na mabadaliko ya teknolojia. Alisema pia Airtel
imeendelea na juhudi za kulete huduma zake karibu kwa wateja ambapo
mpaka sasa tunayo maduka ya Airtel Money Branches Zaidi ya 3,000 nchini
kote ambayo yanatoa huduma na bidhaa zake zote bila mteja kutembea kwa
umbali mrefu.
Wafanyakazi
wa Kitengo cha Huduma kwa wateja wakiongozwa na Mkurugenzi wa Kitengo
hicho Adriana Lyamba (wa pili kulia) na Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni
wakishiriki kwenye kukata keki kuashiria kuzindua maadhimisho ya Wiki ya
Huduma kwa wateja. Airtel imetangaza matukio tofauti ambayo yataambana
na maadhimisho hayo ikiwemo kutoa msaada kwa watoto walio kwenye
mazingira magumu.
Mkurugenzi wa Kitengo cha Huduma kwa Wateja Airtel Tanzania Adrian
Lyamba (kushoto akiongea na Katibu Mtendaji wa Baraza la Ushauri la
Watumiaji wa Huduma za Mawasiliano kutoka Mamlaka ya Mawasiliano
Tanzania Mary Msuya (wa pili kulia) na Meneja Elimu na Uhamashishaji wa
Baraza hilo Hillarly Tesha ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Wiki ya
Huduma kwa wateja. Wa pili kushoto ni Meneja Uhusiano Airtel Jennifer
Mbuya.
Mkurugenzi
Mtendaji Airtel Tanzania Dinesh Balsingh (kulia) akiwa na Mkurugenzi wa
Kitengo cha Huduma kwa Wateja wa kampuni hiyo Adriana Lyamba
wakimsikiliza mfanya kazi wa Kitengo cha Huduma kwa Wateja mara baada ya
kuzindua Wiki ya Huduma kwa wateja. Airtel imetangaza matukio tofauti
ambayo yataambana na maadhimisho hayo ikiwemo kutoa msaada kwa watoto
walio kwenye mazingira magumu.
Monday, October 3, 2022

Airtel yazindua maadhimisho ya Wiki ya Huduma kwa Wateja
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment