HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, October 12, 2022

RAIA WA UGANDA WASEMA UJIRANI MWEMA NA TANZANIA NGUZO MUHIMU MAPAMBANO YA EBOLA



NaFaustine Gimu,Bugango Uganda/Tanzania .
BAADHI ya raia wa Uganda wamesema ushirikiano na ujirani mwema Tanzania umekuwa nguzo muhimu katika kupambana na ugonjwa wa Ebola kwa kuweka mikakati ya pamoja katika kuzingatia kanuni za afya hasa mipakani.

Wakizungumza katika kijiji cha Bugango upande wa Uganda,baadhi ya raia wa Uganda akiwemo Mulikatete Jesca pamoja na Gaspary Kundii wamesema hatua hiyo ya ujirani mwema imekuwa ni msingi mkubwa kwa kusaidiana masuala mbalimbali ikiwemo ikiwemo hatua za kuzingatia kupambana na Ebola.

“Sisi na Tanzania tunaujirani mwema hatuna shida yoyote ,tunapoenda Tanzania tunahudumiwa ,tunanawa na Jick [sanitizer],tunapewa huduma zote za afya bila shida yoyote “amesema Mulikatete.

Nao baadhi ya viongozi wa kijiji cha Bugango kwa upande wa Tanzania akiwemo mwenyekiti wa kijiji Meshack Masumbuko pamoja na mtendaji wa kijiji Anthony Jovenary wamesema wamekuwa na mkakati wa kuitisha mikutano ya pamoja kwa pande zote kwa ajli ya kuwekeana taratibu za kuzingatia kanuni za afya hali ambayo imesaidia kanuni za afya kuzingatiwa mipakani

Kwa upande wake Mganga mkuu mkoa wa Kagera .Dkt,Issessanda Kaniki amesema wameweka mbinu ya pamoja katika utoaji wa huduma na ufuatiliaji wa pamoja tetesi za wahisiwa wa Ebola na ukaguzi wa wasafiri kwa pande zote mbili.

“Tunashirikiana kuweza kutoa taarifa na kutoa huduma iwapo mtu atatokea”amesema Dkt.Kaniki.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad