HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, October 10, 2022

NAIBU WAZIRI WA ARDHI AWATAKA MAAFISA ARDHI KUWEKA MAZINGIRA RAFIKI KWA WAWEKEZAJI

Naibu Waziri wa Wizara  ya Nyumba  na Maendeleo  ya Makazi  Ridhiwani Kikwete akiwa kwenye  banda moja wapo la wajasiriamali kwenye maonesho hayo Kibaha Mkoani Pwani.

Naibu Waziri aa Wizara , Nyumba na Maendeleo ya Makazi Ridhiwani Kikwete akimkabidhi hati ya ardhi  mkaazi wa Kibaha Mkoani  Pwani jina lake halikufahamika.
Mheshimiwa Naibu Waziri  wa Wizara  ya Nyumba na Maendeleo ya Makazi  Ridhiwani Kikwete akiangalia moja ya hati ambazo ziko tayari kwa kupewa muhusika.
Kutoka kushoto ni Naibu Waziri Wizara ya Nyumba  na Maendeleo ya Makazi Ridhiwani Kikwete akisalimiana na  Kamishna wa Ardhi  Msaidizi Mkoa wa Pwani  Hussein  Sadiki  Idd  wakati alipowasili  kwenye maonesho hayo.

Na Khadija Kalili, Kibaha
NAIBU Waziri wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mheshimiwa Ridhiwani Kikwete amesema kusudi la Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan kuanzisha Wizara hiyo ni kusaidia jamii kumaliza migogoro ya ardhi inayowakabili jamii ikiwa ni pamoja na kuweka mazingira rafiki kwa wawekezaji wanaokuja nchini.

Hivyo amewataka Watumishi wa idara ya ardhi nchini kutatua migogoro ya ardhi inayowakabili wananchi na sio kuwaacha wakiendelea kusumbuka na migogoro isiyokwisha.

Amesema hayo leo Oktoba 9 wakati alipotembelea kutembelea Banda la Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi katika mkoa Pwani katika Maonesho ya tatu ya Uwekezaji na Biashara yanayoendelea katika viwanja vya standi ya mailimoja kibaha mkoani Pwani.

Amesema Wizara hiyo lazima iwe suluhisho la migogoro ya ardhi iliyopo katika jamii na sio kuwaacha wananchi wenye migogoro ya ardhi wakiendelea kuteseka katika migogoro mbalimbali inayowakabili.

“Wewe Mtendaji lazima utoke uende kwenye maeneo ukaangalie ni jinsi gani unaweza kusuruhisha migogoro yao ambayo pia hatimaye humwekea mazingira mazuri mwekezaji akilitaka eneo hilo kwa uwekezaji “ alisema Ridhiwani.

“Mheshimiwa Rais Samia amekwishaifungua nchi kwa uwekezaji maana amekwenda nchi mbali mbali duniani kutangaza fursa za uwekezaji tulizonazo hapa nchini amewaita wawekezaji wamekuja nchini kuwekeza kwa lengo kubwa mahususi ili watu waje kuwekeza”

“Ndiyo mnaona wale watu wa SINO TAN ambao wamefungua kongani ya viwanda kubwa sana hivyo idara ya ardhi ijiandae kwa kuweka mazingira rafiki kwa wawekezaji hao sisi lazima tugeuke kuwa wawekea mazingira mazuri ya uwekezaji kwa kumaliza migogoro ya ardhi iliyopo huko ili wawekezaji wakija kusiwepo migogoro” amesema Ridhiwani.

“Yaani kukitokea tatizo kwenye ardhi ya Mwekezaji sisi idara ya ardhi tugeuke kuwa wasuluhishi katika mgogoro huo kwa kwenda kusuluhisha mgogoro huo ili kumsaidia mwekezaji huyo

Amesema wananchi wenye migogoro ya ardhi huja ofisini kwao kutaka msaada ilikutatua migogoro inayowakabili lakini kuna baadhi ya watumishi wa idara hiyo hawawisehemu ya kutatua migogoro hiyo na kusababisha migogoro kuendelea kuwepo katika jamii.

“mtu anakuja anaonekana kuwa na tatizo linalohitaji usuluhishi lakini wewe mtumishi badala ya kuwa suluhisho au kuwa njia ya kumtafutia jawabu la tatizo linalomkabili wewe nawe unakuwa sehemu ya ukwamishaji” amesema Mheshimiwa Ridhiwani.

Amesema kuwa mikoa mingine waige Mkoa wa Pwani kujifunza namna ya walivyojipanga kutatua migogoro ya ardhi inayowakabili wananchi “Mtu anakuja anamgogoro wa ardhi wewe mtumishi unatakiwa uende kutatua mgogoro huo siyo baada ya kukwambia ana ardhi yenye mgogoro wewe unamsikiliza bila ya kumsaidia kutatua mgogoro huo.

Hatahivyo Mheshimiwa Ridhiwani alikabidhi hati za viwanja tano kwa wanannchi waliokamilisha hatua zote za manunuzi Mkoani humo.

Aidha amezungumzia fedha zilizopelekwa kwa katika halmashauri nchini kwaajili ya kusaidia miradi ya uuzaji wa viwanja amewataka kuharakisha uuzaji wa viwanja hivyo ili viuzwe mapema.

“Hatakama ikiwezekana kushirikisha makampuni binafsi au watu mbali mbali watakaoweza kusaidia kushauri ilikutafuta njia nzuri za kuuza viwanja hivyo fanyeni hivyo sisi kama viongozi wenu tutakuwa tayari kuwasaidia kuruhusu muendelee sambamba na kuhakikisha maeneo ya uwekezaji yanapewa kipaumbele na yanawekewa miundombinu ya huduma zote” alisema.

Aidha Kamishna wa Ardhi Msaidizi Mkoa wa Pwani Hussein Sadiki Idd amesemakuwa tayari wananchi 150 wamepatiwa hati za kumiliki ardhi zao huku wengine 300 tayari hati zao ziko tayari na amewataka wajitokeze kwenda kuzichukua .A

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad