WAZIRI WA MAMBO YA NJE WA IRANI AWASILI TANZANIA KWA ZIARA YA KIKAZI - MTAA KWA MTAA BLOG

HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, August 25, 2022

WAZIRI WA MAMBO YA NJE WA IRANI AWASILI TANZANIA KWA ZIARA YA KIKAZI

 Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Mhe. Amir Abdollahian aliwasili nchini jana usiku kwa ziara ya kikazi ya siku tatu na kupokelewa na mwenyeji wake, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula (Mb) katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Jijini Dar es Salaam


Mara baada ya kuwasili nchini, Mhe. Abdollahian alisema, lengo la ziara yake nchini Tanzania ni kuimarisha uhusiano na ushirikiano kati ya Iran na Tanzania katika sekta za kisiasa na kiuchumi.

Nae Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula alimueleza nia ya Serikali ya Tanzania ni kuendelea kudumisha uhusiano wa kihistoria uliopo baina ya mataifa hayo na kuongeza kuwa Serikali ya Awamu ya sita imejidhatiti katika kukuza na kuendeleza Diplomasia ya Uchumi hivyo ni matumaini yake kuwa ujio wake hapa nchini utachangia kuendeleza diplomasia ya uchumi kati ya Tanzania na Iran.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula akimpokea Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Mhe. Amir Abdollahian katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Jijini Dar es Salaam. Mhe. Abdollahian aliwasili nchini jana usiku kwa ziara ya kikazi ya siku tatu.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula akizungumza na Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Mhe. Amir Abdollahian katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Jijini Dar es Salaam baada ya kuwasili nchini jana usiku kwa ziara ya kikazi ya siku tatu
Mazungumzo ya Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula na Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Mhe. Amir Abdollahian yakiendelea katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mkurugenzi wa Idara ya Mashariki ya Kati katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Hemedi Mgaza.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad