HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Saturday, August 20, 2022

Wananchi washiriki zoezi la Sensa kikamilifu kwa kutoa taarifa sahihi- Kawawa

Mkuu wa Wilaya ya Kilwa mkoani Lindi Zainabu Kawawa akitoa vyeti kwa makundi ya jogging yaliyoshiriki bonanza hilo kwenye Uwanja wa Ukote.

Maandamano ya Bonaza liloandaliwa na Mkuu wa Wilaya ya Kilwa Zainab Kawawa.
Mkuu wa Wilaya ya Kilwa Zainabu Kawawa (mwenye kilemba kichwani) akishiriki mazoezi ya kuhamasisha Wananchi kushiriki Sensa.

Na Mwandishi Wetu Michuzi TV Kilwa
MKUU wa Wilaya ya Kilwa mkoani Lindi Zainab Kawawa amewataka wananchi kushiriki zoezi la sensa kikamilifu kwa kutoa taarifa sahihi zitazofanya Serikali kupanga mipango yake katika utoaji wa huduma mbalimbali.

Kawawa aliyasema hayo katika Bonaza la Michezo kwa ajili ya wananchi wa Wilaya hiyo kuungana kwa pamoja katika sensa ya Agasti 23 mwaka huu.

Amesema kwa wananchi walioshiriki ndio watakuwa mabalozi wa sensa katika kufanya kazi hiyo isiyo ngumu kwa makarani wakati wakipita kwenye kaya.

"Rais Samia Hassan Suluhu kawa katika mstari wa mbele wa jambo hili hivyo sisi kama wasaidizi wake ni wajibu kuhamasisha kwa kurti Miz and lengo la Rais na serikali yake kutokana na Sensa hiyo imechukua rasilimali nyingi ya taifa hili"amesema Kawawa.

Aidha amesema kuwa sensa kwa miaka 10 inafanyika mara moja na ndio inapanga mipango ya serikali hivyo kwa sasa wananchi washiriko ipasavyo ili sensa hiyo itaumike kupanga vipaombele vya saaa na baada ya miaka kumi (10) ijayo

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad