HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Saturday, August 20, 2022

Safari ya Meridianbet Kumshika Mkono Mgonjwa Buza

 *Meridianbet Walivyofunga Safari Kumshika Mkono Mgonjwa Buza

UNAPOKUWA katika wakati mgumu, unafaa kuwa na matumaini kuwa kuwa jamii yetu ni bora sana, na changamoto zako sio za kwako peke yako. Andrew Rossi, alifarijika sana kuona nyuso za wana Meridianbet wakigonga hodi nyumbani kwake.


Bwana Rossi, ana changamoto ya kiafya, ambayo alihitaji kiasi cha fedha kwa ajili ya vipimo vya afya na matibabu.

 

Timu ya Meridianbet, ikiwa pamoja na mmoja wa mabalozi wake Jackob Mbuya, waliwasili nyumbani kwa bwana Rossi, baada ya kupata taarifa zake za kuugua na uhitaji.

 

Kupitia programu yao ya “Shinda Penati Uisaidie Jamii Yako”, ambayo mabalozi na wahamasishaji wanakaribishwa kupiga mikwaju ya penati, ambayo kila goli linalofungwa lina thamani ya shilingi elfu hamsini, Mbuya aliweza kucheka na nyavu kwa mikwaju yote mitano aliyocheza.

 

Mbuya, alipewa nafasi ya kuchagua wapi angependa kuielekeza pesa yake aliyoshinda kwenye mikwaju ya penati, ili kuisaidia jamii inayomzunguka. Mbuya, alichagua kuelekeza kiasi cha ushindi wake kwenye matibabu ya Mzee Andrew Rossi, mkazi wa Buza.

 

Meridianbet, waliongeza kiasi cha laki mbili na nusu, kwenye laki mbili na nusu iliyopatikana kwenye mikwaju ya penati kukamilisha kiasi cha laki tano, kilichofikia uhitaji wa vipimo na manunuzi ya dawa ya mgonjwa, pamoja na mahitaji kadhaa ya nyumbani.

 

Mzee Andrew Rossi alitoa shukrani zake kwa Meridianbet “Nawashukuru sana Meridianbet, naamini mungu atawaongeza pale walipopunguza, nimefarijika sana”

 

Meridianbet, ambao ni mabingwa na wakongwe wa uendeshaji wa michezo ya kubahatisha Tanzania, wakiwa na ubashiri wa michezo na kasino ya mtabdaoni, wanataja kuwa hii ni namna bora kwao kuwa karibu na jamii yake.

 

“Naam, hii ni namna ambayo tumekuwa tukiitumia kurejesha kwa jamii. Tunaona kuwafikia wazee na wahitaji wengine kunatuweka karibu na jamii yetu. Tunafahamu hatuwezi kutatua changamoto zote, lakini tunajitahidi kama hivi” – Dickson Richard, kutoka kitengo cha maudhui cha Meridianbet.

 

Twaha Mohamed, kutoka kitengo cha Masoko pia aliongeza kuwa “Kwa wapenzi wa ubashiri, licha ya ukweli kuwa wanajiweka katika nafasi kubwa ya kushinda jackpot za Meridianbet Casino, pia wanaiwezesha Kampuni hii kusaidia umma.”

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad