HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Saturday, August 13, 2022

SERIKALI ZA MITAA, JAMII WAOMBWA WASIWAFICHE WATOTO WASIOONA WAKATI WA SENSA

 MRATIBU wa Idara ya wanawake na watoto wa Chama cha Wasioona Tanzania(TLB), Subira Shedangio ametoa wito kwa jamii kutowaficha watoto Wasioona katika Zoezi la Sensa linalotarajiwa kufanyika Agosti 23 mwaka huu.


Amesema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam Agosti 12, 2022. Amesemakutokuona sio sababu ya kukosa haki za msingi kama haki ya Elimu, afya na ulinzi pamoja na kuhesabiwa wakati wa Sensa.

Amesema kuwa watoto wasioona wasifichwe majumbani watolewe ili waweze kupata haki kwani wanahaki kama watoto wengine.

Amesema watoto wasiiona wanaweza kufanya mambo makubwa.

"Wazazi, Jamii, serikali za mtaa msiwafiche ndani watoto wasiiona waweze kuwato nje, wahesabiwe ili kuirahisishia serikali pamoja na chama cha wasioona Tanzania kuweza kujua mahitaji ya watu wasioona hapa nchini." Amesema Subira
Picha ya pamoja ya wananchama cha watu wasioona Tanzania na Sweden pamoja na wasaidizi wao.
Mratibu wa Idara ya wanawake na watoto wa Chama cha Wasioona Tanzania(TLB), Subira Shedangio akizungumza na waandishi wa habari.
Mratibu wa Idara ya wanawake na watoto wa Chama cha Wasioona Tanzania(TLB), akiwa katika picha ya pamoja na msaidizi wake.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad