Said Mwishehe-Michuzi TV- Zanzibar
MAKAMU
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Kanali Mstaafu Abdulrahman
Kinana amefafanua hatua kwa hatua namna ambavyo Rais Samia Suluhu Hassan
amepatikana, huku akieleza kuwa wanaodai uwepo wake madarakani ni
kutokana na Katiba tu, sio kweli.
Amesema Rais Samia amepita
kwenye mchakato wote kwa mujibu wa Katiba na amepigiwa kura kama ilivyo
kwa mgombea urais na kubwa zaidi Chama Cha Mapinduzi (CCM) kilimpima kwa
sifa zote ambazo anatakiwa kuwa nazo kiongozi wa nchi.
Kinana
ametoa ufafanuzi huo leo Agosti 13,2022 alipokuwa akizungumza na wana
CCM Mkoa wa Kaskazini Unguja visiwani Zanzibar kwenye Kongamano la
kumpongeza Rais Samia Suluhu Hassan kutokana na kutekeleza vema Ilani ya
Uchaguzi Mkuu ya mwaka 2020/2025.
“Nataka niseme na vizuri
Watanzania wakajua tangu Rais Samia achukue uongozi wa taifa letu kuna
kauli nimekuwa nikisikia kuwa Rais Samia ni Rais wa Katiba. Kauli hii
ina ukweli lakini haina ukweli.
“Inaukweli kweli kwasababu Katiba
ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inasema kila chama kitaweka mgombea
na mgombea mwenza na Katiba inasema mgombea Mwenza na mgombea wanafasi
moja ya kupiga kampeni ya chama chao na kila Chama kinatakiwa kuwa na
Mgombea Mwenza,”ameeleza Kinana.
Aidha amesema CCM hakikumchagua
Mgombea mwenza kwa kucheza bahati nasibu ya kutumbukiza halafu uangalie
nani kapata nani kakosa bali wameweka sifa, kwa kuangalia uwezo,
kukubalika , anafaa ,uwezo wa kufanya kampeni, anaweza kuleta kura
nyingi.
Na mwisho wanajiuliza iwapo mgombea kwa sababu yoyote
atakuwa hayupo au ameondoka madarakani je mgombea mwenza atamudu nafasi
ya kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, vigezo vyote hivyo
vilipimwa kwa Samia.
“Anaweza ndio , ana mudu, ndio, anajua kazi
yake ndio, anaweza kufanya kampeni ndio, anaweza kumsaidia mgombea na
kuleta kura ndio. Mwisho iwapo mgombea kwasababu yoyote ataondoka
madarakani kwa njia za kidunia au zake Mwenyezi mungu anaweza kuchukua
nafasi hiyo wana CCM tukajiridhisha ndio anaweza.
“Kwa hiyo kwa
wale wanaosema huyu ni Rais wa Katiba si kweli , Rais Samia Suluhu
Hassan alipimwa kabla ya kupewa hiyo nafasi, bahati nzuri mimi nilikuwa
Katibu Mkuu wa Chama, nilishiriki vikao vya awali mwaka 2015 na wengine
walikuwepo kwenye vikao, hayo maswali yote tulupojiuliza tukasema
anaweza ,ana mudu hiyo kazi, anaongeza kura, ana uzoefu, anakifahamu
Chama Cha Mapinduzi lakini kama anahitajika kuwa Rais anaweza.
“Sasa
unaposema Rais Samia ni Rais wa Katiba hakuchaguliwa sio kweli lakini
kubwa zaidi Rais anapopigiwa kura na mgombea mwenza anapigiwa kura na
kabla haijafika muda wa kupiga kura iwapo mgombea mwenza Mwenyezi Mungu
atamchukua uchaguzi utasimmamishwa.”
Ameongeza “Kwa nini
usimamishwe? Kama kweli yeye ni Rais tu wa Katiba tuendeee kupiga kura
mambo yaishe .Mwaka 2005 tulikuwa na Mgombea mwenza wa CHADEMA Jumbe
Rajab Jumbe mwenyezi Mungu alimchukua , uchaguzi ulisimamishwa, kwanini
ulismamishwa?
"Kwasababu na yeye ana nafasi muhimu hawezi Rais
wa nchi akapigiwa kura au mgombea akapigiwa kura kama mgombea mwenza
hayupo.Nataka nilifafanue hili hao wanaosema Rais Samia ni Rais wa
Katiba hawasemi kweli.
"Rais Samia ni Rais aliyetokana na
mchakato wa uchaguzi Mkuu , alipopigiwa kura Rais Magufuli na Samia
alipigiwa kura hapo hapo kama Rais aliyemtangulia angekuwa ameondoka
madarakani kwa kujiuzulu au kwasababu nyingine yoyote angekuwa Rais
lakini kwasababu za Mwenyezi Mungu Rais Samia amechukua dhamana.
"Kwanini
basi uchaguzi wa Chadema mwaka 2005 ulisimamishwa? Kwasababu wote
wawili Mgombea Urais na Mgombea mwenza wanatokana na utaratibu wa Katiba
uliowekwa kwa hiyo Rais Samia ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania wale wanaosema ni Rais wa Katiba wana ajenda yao,
msiwasikilize."
Amesisitiza wanaosema Rais Samia ni wa Katiba
hawasemi kweli huku akieleza kuhusi upande wa pili kweli ni Rais wa
Katiba kwani Katiba inasema hivi kila Chama kitateua mgombea na mgombea
mwenza.Rais au mgombea anatokana na matakwa ya Katiba ya Jamhurii ya
Muungano wa Tanzania
"Mgombea mwenza ni matakwa ya Katiba ya
Jamhuri ya Muungano , kwa hiyo anateuliwa Samia kuwa mgombea mwenza
ambaye baadae amekuwa Rais kutokana na matakwa ya Katiba kwa hiyo Rais
Magufuli ni Rais wa Katiba.Mgombea unapendekezwa na Chama chako,
uakwenda kwa wananchi lakini hupigiwi kura peke yako unapigiwa na
mgombea mwenza."
Amefafanua zaidi wa hiyo wanaosema Rais Samia ni
Rais wa Katiba hawasemi ukweli." Rais Samia ni Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania.Nchi ya Marekani Rais wa sasa ni Rais wa 46 ,
katika marais 46 waliowahi kufariki kabla ya muda wao walikuwa marais
nane baadae wakachukua wagombea wenza ambao wakawa marais.
"Hatujawahi
kusikia wakiambiwa ni marais wa Katiba, lakini hapa Tanzania wanaotaka
kukoroga mambo wanakwambia Rais Samia ni Rais wa Katiba,"amesema Kinana
alipokuwa anatoa ufafanuzi kuhusu Rais Samia.
Makamu
Mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara, Kanali Mstaafu Abdulrahman Kinana
akizungumza wakati wa kongamano la kumpongeza Rais Samia Suluhu Hassan
lililoandaliwa na CCM Mkoa wa Kaskazini Unguja, na kufanyika Mahonda
Wilaya ya Kaskazini B.
Makamu
Mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara, Kanali Mstaafu Abdulrahman Kinana,
akipokea matembezi ya wana CCM ya kumpongeza Rais Samia Suluhu Hassan,
yaliyofanyika Wilaya ya Kaskazini B, Mkoa wa Kaskazini Unguja. (Picha
zote na Fahad Siraji wa CCM).
Makamu
Mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara, Kanali Mstaafu Abdulrahman Kinana,
akiteta jambo na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Kaskazini, Iddi Ali Ame,
wakati wa kongamano la kumpongeza Rais Samia Suluhu Hassan,
lililoandaliwa na CCM Mkoa wa Kaskazini Unguja na kufanyika Mahonda,
Wilaya ya Kaskazini B, mkoani humo.
Makamu
Mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara, Kanali Mstaafu Abdulrahman Kinana,
akisalimiana na viongozi mbalimbali wakati akiwasili Afisi Kuu ya CCM,
Mkoa wa Kaskani Unguja kulipofanyika kongamano la kumpongeza Rais Samia
Suluhu Hassan, Wilaya ya Kaskazini B, mkoani humo.
Makamu
Mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara, Kanali Mstaafu Abdulrahman Kinana,
akiwa na viongozi wengine wa Chama wakifuatilia kongamano la kumpongeza
Rais Samia Suluhu Hassan, lililoandaliwa na CCM katika Mkoa huo na
kufanyika Mahonda, Wilaya ya Kaskazini B, mkoani humo.
Katibu
wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, Itikadi na Uenezi, Shaka
Hamdu Shaka, akizungumza wakati wa kongamano la kumpongeza Rais Samia
Suluhu Hassan lililoandaliwa na CCM Mkoa wa Kaskazini Unguja, na
kufanyika Mahonda Mkoa wa Kaskazini Unguja. Mgeni rasmi katika kongamano
hilo alikuwa Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara, Kanali Mstaafu
Abdulrahman Kinana.
Vijana
wakifuatilia kongamano la kumpongeza Rais Samia Suluhu Hassan,
lililoandaliwa na CCM Mkoa wa Kaskazini Unguja lililofanyika Mahonda,
Wilaya ya Kaskazini B, mkoani humo. Katika kongamano hilo Makamu
Mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara, Kanali Mstaafu Abdulrahman Kinana,
alikuwa mgeni rasmi.
Saturday, August 13, 2022

Home
SIASA
KINANA AFAFANUA KUHUSU RAIS SAMIA...WANAOSEMA NI RAIS WA KATIBA SIO WAKWELI, WASISIKILIZWE
KINANA AFAFANUA KUHUSU RAIS SAMIA...WANAOSEMA NI RAIS WA KATIBA SIO WAKWELI, WASISIKILIZWE
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment